ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 11, 2011

Kitanda kinahitaji busara, siyo upole wala mapepe - 3-GPL

KILA mtu yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi, isipokuwa watoto na wale ambao Mungu hakuwapa ubongo uliokamilika. Hivyo kwa wale ambao tumepewa fursa yanatugusa, kwa hiyo ni haki tubadilishane uzoefu.

Tunahitaji kujielimisha mara kwa mara kuhusu mapenzi. Haina maana kwamba hujui, la hasha! Inawezekana una uelewa mkubwa lakini huwezi kujaliwa utambuzi wa kila kitu.

Hivyo basi, nakushauri mara kwa mara uwe unapita kwenye ukurasa huu ili uchote japo elimu kidogo ambayo kwa maana moja au nyingine inaweza kuwa tiba ya jambo ambalo linakutatiza.

Wiki iliyopita nilitoa mfano wa Winston Churchill aliyedai kuwa watu wapole wanaoamini katika kuishi kwa utakatifu huwa hawana athari kubwa kwenye jamii. Akaongeza kwamba hata mchango wao huwa ni mdogo.

Ni kweli, nukuu hiyo kwenye mapenzi naieleza kuwa ni busara watu ambao huwa hawataki kujishughulisha kwenye mapenzi mara nyingi hujikuta wakiteseka bure, kwa maana wenzi wao huamua kutoka nje kuangalia wale ambao wanawajibika.

Wakati mwingine watu wanateswa na hisia tu. Wanayavaa maji kwa pupa matokeo yake wanaumbuka. Wanataka kulazimisha ubavu kitandani. Kila mmoja anahitaji amuweze mwenzi wake, badala ya kujenga hisia za kuridhishana. Yaani wewe utamani kumfurahisha na siyo kumkomoa.

Hali kadhalika, naye pia awe na hisia za kukuridhisha. Asiwe na mawazo ya kukuchezesha ligwaride au kukukomoa ili akajisifie. Mapenzi hayapo hivyo, wenye hulka hiyo ni malimbukeni.

Mapenzi ni starehe, siyo mapambano ya ana kwa ana kusema lazima mmoja aibuke mbabe. Hisia hizo ndizo ambazo zinawafanya wengi waumbuke. Wanatumia nguvu nyingi katika tendo linalohitaji nafasi.

Siku zote unapoingia kitandani unapaswa kujiamini. Baada ya hapo chukua muongozo wa kuheshimu hisia za mwenzi wako. Naye pia unatakiwa kumuamini kuwa atakupa kitu kamili. Amini katika matokeo chanya.

Wanasema mkamia maji hayanywi. Kwa maana mtu anayeendekeza kiu na kufakamia maji ili anywe mengi, matokeo yake hata glasi hakumaliza. Alibaki anayatazama kwa jicho la mshangao. Yamemshinda nguvu.
Mambo yafuatayo, yataondoa mapepe na kujenga busara halisi ya kitandani.

PUMUA BAADA YA MSHINDO
Kitanda siyo gym, ni eneo la starehe. Viungo vya mapenzi siyo vifaa vya mazoezi kusema unaweza kuvitumia wakati wowote. Kawaida yake ni kwamba huwa vinahitaji muda wa kutosha baada ya kufika mshindo ili kukaribisha hisia.

Kuna wanawake hulazimisha kuunganisha. Ni sawa lakini ni vizuri kuheshimu hisia kuliko kuyavaa magoli yasiyo na msisimko wowote. Unataka kuonekana unamudu kupambana kwa muda mrefu? Hiyo siyo sifa kama unavyoweza kudhani.

Kupumua baada ya mshindo mmoja na kungoja mwili ukuruhusu awamu nyingine ndiyo utaratibu wa kijanja. Kwa wanaojua maana ya mapenzi na starehe zake watakuona mshamba kama utakuwa unang’ang’aniza kuunganisha.

KUJISTIRI MUHIMU
Utakwenda mshindo mmoja, kurudi awamu ya pili inaweza kuwa ngumu. Unadhani wewe ni mgonjwa? Hapana, maungo ya mwenzi wako umeyazoea sana, kwa hiyo hayakupi msisimko. Lile la kwanza ni kwa sababu ya mguso wa kimaumbile ndani kwa ndani.

USIFUMBE MACHO
Tabia yako ni kufumba macho wakati unakabiliana na mwenzi wako faragha? Unakosea. Mapenzi yanakusisitiza umtazame mwenzako,mbadilishane hisia ikiwezekana mwisho wa safari mfike pamoja. Hiyo ni nidhamu kubwa katika mapenzi.

2 comments:

Anonymous said...

Dj luke bado unapenda .yanga kama zamani.ulikuwa mshabiki.mzuri sana mpaka unamkaribisha.lunyamila nyumbani.sio mchezo.mazoezi yanakusaidia.hata mwenyewe.ndio maana .umekuwa gulamali wa dc.hiyo poa .maisha ni haya haya.

Anonymous said...

HALOOOOOOOOOOOO WAPE WAPE WAPE HAO WANAOJIFANYA 'OOH LEO MPAKA HATOTEMBEA!!!! HEE ADHABU? WAKATI TUKIMALIZA TUTEMBEE TWENDE BEACH KIDOGO.. SIO BAADA YA SHUGHULI MTU UNAANZA KUJIKANDA MAJI MOTO!! USHAMBA SANA