Mrisho Ngasa(kulia) akiwa na Alex Kajumulo mara tu alipotua uwanja wa ndege Seattle,Alex Kajumulo nae alikua Tanzania wamekuja na ndege moja na Ngasa na wameingia jana Seattle na leo Mrisho Ngasa alitarajia kuanza mazoezi ya majaribio na timu ya Seattle Sounders na moja yamajaribio ni kucheza mechi ya Man U wakati Seattle Sounders watakapocheza na Shetani wekundu hao July 23,2011,Alex Kajumulo ameomba Watanzania Wote Tumuombee kwa Mungu kwani mafanikio yake ni mafanikio ya Watanzania wote na atakua amefungua milango kwa wachezaji wengine na kutangaza jina la Tanzania kwenye medani ya soka hapa Marekani na kwa wapenda soka Duniani.(picha kwa hisani ya Alex Kajumulo)
No comments:
Post a Comment