Makala hii ni muendelezo wa makala iliyokuwa inazungumzia mambo ya ndoa na matatizo yake, endelea.
NDOA
UCHUMBA ni hatua muhimu sana katika kuelekea katika maisha ya ndoa. Ni kipindi ambacho ni muhimu kwa kupata fursa ya kujuana vema kabla hamjaingia katika ndoa. Hivyo unahitajika umakini wa hali ya juu katika kipindi hiki ili kuepusha mateso na maumivu ndani ya ndoa kwa kuwa na mume au mke ambaye hakuwa chaguo lako muhimu.
NDOA
UCHUMBA ni hatua muhimu sana katika kuelekea katika maisha ya ndoa. Ni kipindi ambacho ni muhimu kwa kupata fursa ya kujuana vema kabla hamjaingia katika ndoa. Hivyo unahitajika umakini wa hali ya juu katika kipindi hiki ili kuepusha mateso na maumivu ndani ya ndoa kwa kuwa na mume au mke ambaye hakuwa chaguo lako muhimu.
Kabla ya kuingia moja kwa moja katika ndoa na mchumba wako huyo, kuna mambo ya msingi ya kuyazingatia na kuyajua juu ya huyo mtu maana ni heri kuvunja uchumba na mtu ambaye hafai, kuliko kuingia kwenye ndoa yenye maumivu na mateso kila kukicha.
Hapa chini ni baadhi ya mambo ya kuzingatia.
Uchaguzi sahihi
Hili ni suala muhimu sana katika uchumba maana kuna baadhi ya watu wanaingia katika uchumba kwa vigezo binafsi au kwa sababu ni maarufu au ni tajiri, sasa kwa kuzingatia mantiki hiyo anakuwa hajampenda kwa dhati, hili ni tatizo kwani mwisho huwa ni maumivu katika ndoa na usaliti.
Kati ya vitu muhimu maishani ni pamoja na kuwa na mwenzi sahihi katika ndoa hivyo kabla hujaoana na huyo mchumba wako, basi ni lazima ujiridhishe kama kweli una mapenzi ya dhati juu yake.
Historia yake.
Baada ya kujiridhisha kuwa ni kweli una mapenzi ya dhati juu yake, sasa ni wakati wa kumjua kwa undani zaidi, yaani ujue kwanza historia yake ya huko nyuma kabla hamjafahamiana. Ujue maisha yake ya kimapenzi kabla ya kukutana kwenu na upate nafasi ya kuifahamu zaidi familia yao.
Hapa namaanisha kwamba epuka sana kuwa na mchumba ambaye huijui familia yake kwani yaweza kuwa ni tatizo kwa kutojua angalau kwa kifupi maisha ya familii yao, nina maanisha maadili ya familia yao yakoje?
Kumsoma.
Hatua hii ni ya kuzingatia sana kwani baada ya kuridhika na historia yake, maadili ya familia yake na mambo mengi yanayohusiana, sasa unatakiwa uanze kumsoma mchumba wako kuwa anapendelea nini na hapendelei kitu gani, yaani ujue kwa undani ni mtu wa aina gani na utaishi nae vipi hasa mkishaingia katika ndoa yenu ili kuepusha migongano ya mara kwa mara ndani ya ndoa.
Kujali
Ni lazima sasa uioneshe kumjali mchumba wako huyo, maathalani wewe ni mwanamke na unaishi karibu na mchumba wako si jambo baya kama utakuwa unaenda mara moja moja kumfulia nguo nyumbani kwake, kumpikia, na hata kumfanyia usafi wa ndani ya nyumba anayoishi.
Kwa mwanaume, mnunulie zawadi au kula naye chakula. Hii itamfanya ajione wa pekee kwako na atakupa thamani ya juu sana kwani ataona unamjali kwa vitendo.
Kuheshimiana.
Hapa ni lazima uoneshe ni jinsi gani unamheshimu kama mwanandoa wako mtarajiwa na umpe thamani yote kama mume au mkeo na katika hili hutakiwi kuwa na heshima ya kulazimisha na kuiga, ni lazima uwe na heshima ambayo ni dhati na epuka kejeli na dharau kwake na kwa familia yake.
Ndugu zangu ndoa ni jambo la pekee na ni zawadi maalumu kutoka kwa Mungu.
MUHIMU ZAIDI
Epuka mapenzi ya kujaribu na usiingie katika ndoa kwa mkumbo eti kwa sababu fulani kaolewa au kaoa.
1 comment:
ukikosea kuchagua utajuta unajua unaweza kuoa hata leoleo lakini kuamua leo leoleo kumuacha mkeo ni ngumu na haiwezekani maana ataenda hata kwa pilato ila mchumba hana taraka hata kwa pilato hawaendagi na wakienda hawashindagi kuwa makini na chagua umpendaye kweli na anayekufaa kweli usichanganywe na hips au kalolaiti huwavinapotea hivi muda mfupi tu.
Post a Comment