Kasesela akionyesha fulana moja ya fulana atakayotoa kwa timu mshindi ya pambano la Simba na yanga litakalochezewa Manassas,Virginia Jumamosi Sept 24,2011 kugombea Uhuru Cup
Homa yazidi kupanda miongoni ya wachezaji na mashabiki wa Simba na Yanga kuhusu mtanange utakaochezwa kesho Jumamosi ya September 24,2011 kugombea kombe la Uhuru,mechi itakayoshuhudiwa na mashabiki wa pande zote mbili wapatao 600 kutoka Tanzania na Marekani nzima inatarajiwa kua ya upinzani mkali kwani hakuna timu itakayokubali kufungwa kirahisi na kama itatokea suluhu,zitapigwa penati tano tano.
Kocha wa Simba amesema kesho timu yake itatumia formation ya 4-6-0 amayo anaamini itawasumbua Yanga kwa sababu mabeki wa timu hiyo ya Jangwani hawatajua nani wa kumkaba
Kocha wa Yanga Yasini Manyoka amesema kwamba wachezaji wake wapo fiti na tayari kwa mchezo huo na Yanga wanapoona Kombe uwanjani hua mbogo,Simba kipigo ni lazima yaliyotokea Columbus,Ohio kwa Simba kuibuka mshindi wa 5-2 ndio itakua chachu ya Ushindi wa Yanga amewaomba mashabiki wote wa Yanga watakaokuja kushuhudia mtanange huo wavae nguo za kijani na njano,Kombe la UHURU ni letu.
German Defense(Libe) amesema Ohio Yanga waliongea tukawapiga bao hata mechi hii waache waongee tukiingia tu sisi tunafanya kweli, Yanga ishaelekea kibla kilichobaki ni kuchinjwa tu,"nasikia Yanga wamewaagiza mashabiki wao kuvaa nguo za rangi ya jangwani" ,Mashabiki wa Simba mnajua kitu gani cha kufanya na sisi tuvae nguo nyekundu na nyeupe.
Mechi inatarajiwa kuanza 4:30pm kwa hiyo wachezaji wote mjitahidi mfike uwanja kwenye 4:00pm
a mechi hii kwa mara ya kwanza itachezewa Manassas,Virginia,The Splashdown Waterpark
7500 Ben Lomond Park Dr,
Manassas,VA,20109
Nyama choma kwa wingi usisahau TOOTHPICK
POMBE NI MARUFUKU KWENYE HII PARK
No comments:
Post a Comment