Kwa Wanajumuiya
Kwanza napenda kuwapa salamu kutoka Washington,DC. Kwa hakika shughuli ilikuwa ni nzuri sana na tumefarijika kupita kiasi. Watu wa North Carolina wengi walijitokeza kwenda na naamini na wao pia wameona kama nilivyoona mimi ( angalau sura zao zilionyesha furaha na tabasamu kwa muda wote)
Ni shauku yangu kuona katika mazuri haya yamekamilika kwa ushirikiano wa Wanajumuiya wangu.Dr.Kurwa Nyigu na Nisa Kibona ni miongoni mwa walioshiriki katika maandalizi ya sherehe kubwa hii-Ahsanteni sana kwa uwakala mzuri katika mambo mazuri kama haya.
Safari hatua; Kuna ambao walipendelea kuhudhuria, kwa bahati mbaya wakapatwa dharura na kushindwa kuhudhuria. Tunasikita sana na poleni sana.
Ni Imani yangu wengi watazidi kujitokeza kushiriki katika mambo ya maendeleo kama haya na hata kushika nafasi za Uongozi wa vyombo kama hivi.
-Tuendelee na matayarisho ya uchaguzi; Nashukuru sana kuona mapendekezo ya kutaka mimi nigombee tena, ila nasikitika sana kuwajulisha sitowezakugombea. Kafuatana na majukumu binafsi na ya kifamilia naomba mniwie radhi na wengine tujitokeze kugombania kukiimarisa chombo chetu.
Wapo watu wengi wenye uwezo.
Ahsanteni nyote
Nassor Ally,Chairman
UTNC & TCLA
P.O.Box 52531
Durham,NC 27717
Maendeleo ni haki ya wenye kuyapigania, hayaji
bila nguvu za makusudi na zenye muelekeo.
Shirikiana na wenzio kwa kuijenga jamii yako
Shirikiana na wenzio kwa kuijenga jamii yako
No comments:
Post a Comment