Pichani Juu na Chini Mgeni rasmi Hoyce Temu akiwapa risala wahitimu wa kidato cha IV katika shule ya Cambridge. Hoyce aliwasihi wahitimu hao kuhakikisha kuwa wanafanya mitihani yao kwa utulivu na kujiamini sambamba na kuwasisitiza kuchagua masomo yenye masoko katika ajira na kujiendeleza binafsi. Aidha aliwaomba wazazi na walezi kuwasaidia vijana hao katika safari yao ya Maisha na kuwataka kuwa wavumilivu wakati wote ili waweze kufikia mafanikio
Mgeni rasmi Bi. Hoyce Temu akishukuru kwa mchango wa Sesilia aliokabidhiwa baada ya harambe ya haraka haraka kupita kwa wageni waalikwa katika mahafali hayo.
Mwanafunzi Monica Mwaipopo akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi Hoyce Temu cha kufanya vizuri katika taaluma na Vilabu Shuleni hapo.
Naye mwanafunzi Rose Nawander akipokea cheti cha kuwa mwanafunzi bora kwa upande wa taaluma na vilabu vya dini kutoka kwa mgeni rasmi Hoyce Temu.
Meneja wa Shule ya Sekondari Cambridge Bi. Laura Mataita akihamisha uchangiaji wa fedha za Mtoto Sesilia Edward ambaye anasumbuliwa na maradhi ya moyo anayetarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu. Mtoto Sesilia aligundulika kufuatia kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Channeli Ten na kuendeshwa na Hoyce Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule hiyo.
Umati wa wageni waalikwa, walezi na wazazi waliohudhuria mahafali hayo ya kumi na moja shuleni hapo.
JAPO NI KIDOGO TUNAKUOMBA UZIWASILISHE KWA SESILIA, ndivyo anavyosema Meneja wa Shule ya Sekondari Cambridge Bi. Laura Mataita wakati akimakabidhi mgeni rasmi na Mwendeshaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Bi. Hoyce Temu.
Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 11 akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Cambridge.
Wahitimu wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Cambridge wakiingia rasmi katika sherehe za mahafali yao kwa wimbo maalum. Sherehe hizo zilifanyika Shuleni hapo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali pamoja na ndugu na jamaa.
No comments:
Post a Comment