Mshehereshaji katika sherehe za kufungwa kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru na Utoaji huduma za Afya Tanzania MC Peter Mavunde zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara na Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini
Baadhi ya Wafanyakazi wa Idara mbalimbali za Wizara ya Afya wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara hiyo. Mhe. Lucy Nkya.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara na Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin.
Burudani ya Muziki kutoka kwa Mjomba Bendi katika kunogesha sherehe za kufungwa kwa maadhimisho hayo.
Burudani ya Muziki kutoka kwa Mjomba Bendi katika kunogesha sherehe za kufungwa kwa maadhimisho hayo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Idara mbalimbali za Wizara ya Afya wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara hiyo. Mhe. Lucy Nkya.
Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin akizungumza wakati wa kufungwa kwa maadhimisho hayo ambapo ameipongeza Tanzania kwa Mafanikio iliyofikia katika utoaji huduma za Afya katika Kipindi cha Miaka 50 iliyopita haswa katika kupunguza vifo vya watoto wadogo ambapo Tanzania kwa sasa imefanikiwa kupunguza vifo 110.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Dkt. Lucy Nkya akitoa hotuba ya kufunga maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru na Utoaji Huduma za Afya Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia mafanikio yaliyofikiwa katika kutoa huduma ambazo hazikuwa zikipatikana hapa nchini kama vile Tiba ya Mfupa na Viungo, Upasuaji wa Moyo, Saratani na Tiba ya Magonjwa ya Figo pamoja na kusafisha Damu.
(picha kwa hisani ya www.mohammeddewji.com/blog)
Kwa picha zaid na maelezo Bofya Read More
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya (katikati) katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Afya na Serikali.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya akielekea kukagua mabanda yaliyokuwa yanatoa huduma za Upimaji na Matibabu Bure kwa Wananchi wote.
Mgeni rasmi akiongea na baadhi ya Wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma za Upimaji na Matibabu ya Masikio, Koo na Pua.
Mhe.Lucy Nkya akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi Blandina Nyoni (kulia) wakizungumza na Muuguzi kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Kitengo cha Uchunguzi wa Awali wa Saratani ya Kizazi Maria Haule (kushoto).
Mgeni rasmi akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma ya upimaji na matibabu bure wakati alipotembelea mabanda yanayotoa huduma hizo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Chama cha Maalbino nchini akitoa maelekezo kwa Mhe. Naibu Waziri juu ya Dawa wanazotumia walemavu wa ngozi kwa ajili ya kujikinga na madhara ya mionzi ya jua.
Mganga Mtafiti wa Tiba Asilia na Magonjywa Sugu na Ukimwi Tanzania kutoka M.M.D.K Dkt. Ahmadi Darusi Salim akitoa maelezo kwa Mhe. Mgeni Rasmi ya Dawa inayotumiwa na Wagonjwa waliothirika na Virusi vya Ukimwi kwa ajili ya kuimarisha Afya zao. Ambapo mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya alimshauri kupeleka dawa wanazozitafiti katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ili kuhakikiwa.
Meneja Habari na Ushauri wa Taasisi ya John Hopkins Centre For Communication Programme Tanzania Fauziyat Abood akitoa ufafanuzi wa Shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo kwa mgeni rasmi alipotembelea katika banda hilo.
Mgeni rasmi na Ujumbe wake wakipata maelekezo kutoka kwa Sada Nabos Nachundu wa Nzasa W. Group wanaotengeneza bidhaa mbalimbali za lishe kwa kutumia unga wa zao la Mtama.
No comments:
Post a Comment