Mama Maria Nyerere akiwa kwenye picha ya pamoja na mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kimataifa wakati walipotembelea kaburi na makazi ya Hayati Baba Mwalimu Julius Nyerere katika kijiji cha Butiama mkoani Mara jana. Waliokaaa kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mabalozi, Balozi Juma Mpango, anayemfuatia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupa, pamoja na Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe. Kulia ni mtoto wa Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere. Pichani juu: Mama Maria Nyerere( katikati) akiwa na Kiongozi wa Mabalozi hapa nchini Balozi Juma Mpango (wa kwanza kulia) wakiomba dua kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kijijini Butiama jana wakati mabalozi hao walitembelea makazi na kaburi la Mwasisi huyo wa taifa la Tanzania. Wengine katika picha wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa, Waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe wakati wa pili kulia ni mwanae Charles Makongoro Nyerere.
Baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kimataifa yaliyopo nchini wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikisomwa na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe wakati walipotembelea kaburi na makazi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kijiji Butiama, mkoani Mara.
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akisalimiana na Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe wakati alipotembelewa na ujumbe wa mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kijijini kwake Butiama, mkoani Mara jana. Anaangalia kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mara, John Tupa na kutosho juu ni mtoto wa Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere.
Picha na Anna Itenda - Maelezo
No comments:
Post a Comment