MAPENZI ni matamu lakini siyo rahisi. Mada hiyo niliyoiandika kwenye gazeti hili kwenye matoleo yaliyopita ndiyo imeleta muendelezo huu. Hii ni sehemu ya pili na lengo lake ni kuushinda ugumu uliopo na kuyaweza mapenzi kwa asilimia 100.
Jambo la muhimu ni kwamba usije ukaingia kwenye uhusiano ukidhani kila kitu ni chepesi. Unatakiwa kujipanga, halafu uwe mdadisi kisha upite njia inayostahili.
Ugumu mkubwa ambao upo kwenye mapenzi ni pale mtu anapotaka aoneshwe upendo kulingana na jinsi anavyopenda. Inapotokea anabaini tofauti kati ya anavyopenda na anavyopendwa inakuwa shida kubwa. Hataki kupenda zaidi, eti ataonekana wa bei nafuu.
Jambo la muhimu ni kwamba usije ukaingia kwenye uhusiano ukidhani kila kitu ni chepesi. Unatakiwa kujipanga, halafu uwe mdadisi kisha upite njia inayostahili.
Ugumu mkubwa ambao upo kwenye mapenzi ni pale mtu anapotaka aoneshwe upendo kulingana na jinsi anavyopenda. Inapotokea anabaini tofauti kati ya anavyopenda na anavyopendwa inakuwa shida kubwa. Hataki kupenda zaidi, eti ataonekana wa bei nafuu.
Kila mtu anataka apendwe zaidi. Kwa nini wewe usiwe wa kwanza kujitoa kumpenda mwenzi wako kuliko yeye anavyokupenda? Ni mtihani mdogo lakini unawashinda wengi na kusababisha mvutano.
Uzoefu unaonesha kuwa watu wengi hawana imani na wenzi wao. Dosari ndogo inaweza kuwafanya wajenge imani kuwa wenzi wao hawawapendi. Kila mmoja analalamika kivyake. “Hanipendi kama mimi ninavyompenda.” Ugumu wa mapenzi huanzia hapo.
Nimeshachambua mengi huko nyuma. Kwa nyongeza, leo nakutaka ujiulize maswali yafuatayo ili uepukane na ugonjwa wa moyo, badala yake, mapenzi kwako yawe kitu rahisi ambacho utakimudu kwa asilimia 100.
Tazama unavyojisikia pale unapopenda. Je, unapopenda unajisikia vizuri hata kama umpendaye hakupi upendo kama ulionao kwake? Je, kumpenda mtu, ni lazima naye akupende kwa kiwango hicho hicho? Kama ndivyo, ni kwa nini?
*Unajisikia unapendwa hata kama mwenzi wako hayupo? Kama sivyo, ni kwa nini? Je, unajikubali na unaridhika kwa sifa ulizonazo?
*Unafanya vitu kwa ajili ya mpenzi wako? Hata kama hutaki kufanya, je unajitahidi kutekeleza ili kuliweka penzi lenu hai? Unafanya kwa ajili ya mapenzi yake na unahitaji kila unachofanya, naye akufanyie hivyo hivyo?
*Je, umewahi kumueleza mwenzi wako vitu ambavyo ukifanyiwa vinaweza kukufanya ujisikie kupendwa? Amewahi kutekeleza vitu hivyo kwa ajili yako? Kama bado, umewahi kuvumilia na
kumfundisha taratibu?
MNAFANANA?
Swali hili lipe uzito. Inawezekana kwenye maswali ya juu ukawa umevuka vizuri. Pamoja na hivyo, haioneshi kama kuna mambo ambayo wewe na mwenzi wako mnafanana. Kama hamuendi sawa, jifunze kumuelewa.
Unaamini katika sanaa, mwenzako anadatishwa na michezo. Unapenda kusoma vitabu na kutoka kwenye matembezi ya hapa na pale, lakini yeye anapenda kusafiri. Hata hivyo, unapaswa kuamini kwamba ndoa ni kujitoa muhanga.
Siyo sawa na kutoa na kuchukua. Inatakiwa uwe mwelewa, katika kuhakikisha mapenzi yenu yanafanikiwa, ni vizuri ukahifadhi mambo yako kisha ukaungana naye kwenye mambo yake. Baadaye utamfanya aungane nawe kwako taratibu.
Hilo litafanikiwa kama utaacha ubinafsi. Tabia ya kutaka upendwe zaidi ni kosa. Katika uhusiano hutakiwi kujifikiria wa kwanza. Wekeza upendo mkubwa, halafu umfanye naye akupende. Si kwa haraka, bali taratibu.
Kama kila unaloamini wewe yeye yupo mbali, jifunze mambo yake kwanza. Muelewe kisha mshirikishe yako. Leo ukimfanya ajue kwamba unapenda kuogelea, keshokutwa mpe lingine na umjulishe kuwa ungependa mwende pamoja.
Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment