ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 11, 2011

NYUMBA YA JAMBAZI SUGU YAVUNJWA NA KUCHOMWA MOTO MKOANI IRINGA

Baadhi ya mali zilizokutwa ndani ya nyumba hiyo.
Wananchi wakifukua mali zilizokuwa zimefichwa shimoni na jambazi hilo.
WANANCHI wa  eneo la Mawelewele katika Manispaa ya Iringa  leo asubuhi wamevamia nyumba ya Bw. Msafiri Ilomo ambaye anadaiwa kuwa ni jambazi akihusishwa na vitendo vya kupiga nondo watu na kupora mali zao.  Vile vile Msafiri pamoja na kundi lake wanadaiwa kuhusika na mauaji ya watu kadhaa wa eneo hilo.
Vitu mbalimbali vilivyokuwa shimoni humo.
Zoezi la kufukua mali likiendelea.

Nyumba na vyombo vya jambazi vyachomwa moto Iringa
Ndugu wa karibu wa mtuhumiwa wa upigaji nondo katika eneo la Kata ya Mkwawa na Mlandege katika Manispaa ya Iringa wakiwa chini ya ulizi wa polisi baada ya wananchi na polisi kufanikiwa kuvunja ngome ya ujambazi eneo la Kigamboni mjini Iringa leo.


Mwananchi mwenye hasira kali mkazi wa Kigamboni kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa akivunja nyumba ya jambazi sugu Msafiri Ilomo aliyetolewa kwa msahama wa Rais na kuonyesha kuwatesa wananchi kwa kuwapiga nondo na kupora mali zao
 
Gari la polisi wilaya ya Iringa likibakia vyombo mbali mbali zinavyodaiwa kuwa ni mali za wizi ambavyo vilikutwa katika nyumba ya jambazi sugu Msafiri Ilomo mkazi wa Kigamboni mjini Iringa ,mali ambazo zinadaiwa kuporwa na kundi hilo la ujambazi baada ya kuvunja na kujeruhi wananchi mbali mbali kwa nondo
Wananchi wa Kata ya Mwangata na kata ya Mlandege katika Manispaa ya Iringa wakitazama nyumba ya Msafiri Ilomo ikiteketezwa kwa moto baada ya wananchi kuamua kuivunja nyumba hiyo na kuichoma moto baada ya kukutwa mali mbali mbali ambazo majambazi hao walikuwa wakipora kwa wananchi baada ya kuwapiga nondo mali zenye thamani ya zaidi ya milioni 15

Picha na Francis Godwin na hisani ya FULL SHANGWE

No comments: