ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 10, 2011

Unyumba ni nguzo ya penzi, ukiwa mchoyo unabomoa-2

WIKI iliyopita tulianza kuzungumzia mada juu ya umuhimu wa unyumba kati ya watu wanaoishi kwenye uhusiano wa kimapenzi. Wiki hii tunaendelea kuanzia pale tulipoishia.

“Huyu mbona yupo hivi, kila siku anasema kachoka, atakuwa na mtu huko nje,” ni kauli ambayo ni rahisi kupita kichwani kwa mwanamke, pale anapokabiliana na mwenzi ambaye haguswi chochote na tamaa za mwili, ingawa inaelezwa kwamba ni moja ya kumi ya wanawake ndiyo hukosa usingizi kwa kunyimwa tendo.


Wakati ipo hivyo kwa upande huo, utafiti unaeleza kuwa wanaume wengi huwa hawakubali neno “nimechoka” ambalo anaweza kuambiwa na mwenzi wake. Inaelezwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye ndoa ambao walijaribu kueleza hisia zao kwa ‘mamista’ wao kuwa hawapo tayari kwa tendo, walibakwa.

Inawezekana hili likawa halipati kujadiliwa sana kwa sababu mpaka leo kuna wanawake bado wanaamini kubakwa na waume zao ni sawa. Kinachowapa unyonge huo ni imani kwamba mwanaume ana haki zote za kimsingi za kuutawala mwili wake. Ziangalieni nyumba nje ya kuta, ndani kuna mengi!

Ni vizuri kujitambua. Mfumo wa kubakana haukubaliki! Watu waelewe kuwa ni kosa kubwa kubana unyumba, kwani wengi wao wamejikuta wakisalitiwa kwa sababu hiyo. Yapo mambo ambayo natakiwa nikuchambulie ili kufahamu thamani ya tendo ili uelewe tofauti ya chumvi na sukari.

Mapenzi ni tendo la furaha. Wakati wa utekelezaji huwa ni sherehe tupu endapo wahusika watakuwa wamekubaliana kwa moyo mmoja. Yaani hisia zao ndizo zilizowashawishi kuingia kwenye ‘bwawa spesho’. Kinyume chake ni mateso na ndiyo chimbuko la tuhuma za wanandoa kubakana.

 “Mwanamke akiolewa haruhusiwi kulala akiwa amevaa kabati!” Ni msemo ambao unavuma mno. Kinachotajwa hapo ni kuwa anayekubali kuolewa, moja ya masharti ni kukubali ombi la mwenzi wake wakati wowote. Ni kweli? Usiku amelala, ghafla anashtuka uzito umeongezeka kifuani, kuangalia, kumbe ni mume anatimiza haja zake!

Hiyo ni sahihi? La hasha, mapenzi hayapo hivyo! Nimesema kuwa tendo la mapenzi linahitaji uhuru wa hisia. Kulazimisha ni kumuumiza. Kukwea juu ya mwenzako bila taarifa ni unyanyasaji. Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu mwili wa mwenzake na azitangatie ‘u-tayari’.

Ni vizuri kujitambua. Mfumo wa kubakana haukubaliki! Ila ni vema pia watu wakaelewa kuwa ni kosa kubwa kubana unyumba, kwani wengi wao wamejikuta wakisalitiwa kwa sababu hiyo. Yapo mambo ambayo natakiwa nikuchambulie ili kufahamu thamani ya tendo!

UTAPOTEZA MVUTO WAKO
Tendo ni chachandu! Kwa wanandoa au wapenzi ambao wanaliheshimu hili na kulitekeleza kwa kiwango bora, huwafanya wenzi wao wawe na hisia za karibu kila wanapowafikiria. Hii inamaana ya kuongeza mvuto!

Mtu ambaye anakuwa mvivu kutekeleza, mwisho wa siku hupoteza mvuto wake. Kwa asili kila binadamu huwa hapendi usumbufu. Alihitaji penzi la amani, ndiyo maana akawa na wewe, lakini kwa kitendo chako cha kutotaka ‘kachumbari ilike’, maana yake unampa mateso aliyoyakimbia.

Anakuomba leo, unamjibu umechoka, kesho tena unaweka ngumu! Hasara kwako hapo ni  kupoteza mvuto wa kimapenzi, kwa maana atakapohisi kuhitaji tendo, kila akikufikiria, ataona wewe ni mtata na hueleweki, kwamba akikuomba utamtolea nje.
Kwa mwanamke ni hatari zaidi, kwani kwa wanaume wasio na uvumilivu, mwisho wa siku huishia kubakwa. Hata hivyo, mara nyingi hiyo haiishii hapo, tatizo hukua zaidi na zaidi kulingana na jinsi mgogoro wa kuwekeana ‘kauzibe’ unavyoshamiri ndani ya nyumba.

Ukiweza kumudu kumfurahisha mwenzi wako, anachokihitaji ukimpa kwa wakati. Maana yake atazidi kukuona lulu. Kila akiwa na wewe atajiona yupo huru kuomba huduma wakati wowote. Na pale utakaposema umechoka, itakuwa rahisi kukuelewa na kukuvumilia, kwani siyo kawaida yako.

KUSALITIWA NI NJE NJE
Unambania kila siku, aendelee kukusubiri kwa kitu gani hasa? Kama ni mwanaume, maua yapo mengi ‘kitaani’, kwahiyo ataangalia kwingine kwa lengo la kutuliza mizuka yake. Ni vema ukitambua ya kwamba huyo siyo amoeba! Ni mtu hai anayehitaji huduma.

Kisaikolojia, ni mwanaume mmoja kwa mia, anayeweza kuvumilia kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi. Asili ya maumbo yao, hasa walio na afya timamu, hisia zao zipo karibu, kwa maana hiyo anaweza kuhitaji hata kila siku. Kama ni mwanamke, ni busara kulitambua hili.

Mwanamke anaweza kukaa muda mrefu bila kutamani tendo, lakini hatari kubwa ni kwamba uwezo wake wa kuvumilia ni mdogo mno pale anapokuwa jirani na mwanaume. Akiwa peke yake ni sawa, ila akiwekwa jirani na watu wa jinsia ya pili, mambo huenda kinyume chake.

Unafika nyumbani unalala mzungu wa nne, lakini kuna wakati ukigeuka na kumgusa, unamfanya ahisi kutaka huduma. Wewe unambania, hapo utamsababishia akiamka, afikirie mahali ambapo anaweza kupata tiba! Kwa muuza bucha, genge au hata houseboy!

Itaendelea wiki ijayo.

www.globalpublishers.info

No comments: