BI MOSI katikakti picha juu akiwa na mumewe waliandaliwa huzuru hiyo na wanajumuiya wa New York City kama ishara ya upendo juu yao kutokana na jinsi alivyoishi nao na kushirikiana kwa kila jambo akiwa hapa, Huzuru hiyo ilihuzuliwa pia na viongozi wa jumuiya ya Watanzania waishio New York City na vitongoji vyake, na pia kwa upande wa Ubalozi uliwakirishwa na mama Rose Mkapa..Bi Mosi anarudi Nyumbani Tanzania na moja kwa moja baada ya kuishi New york kwa miaka isiyo pungua 25. Na akiwa Tanzania ataelekea kwenda kuishi katika kitongoji cha Vikokotoni huko Zanzibar wanajumuiya watamkosa sana mama huyu kwani alikuwa ni mpikaji mzuri sana wa vitumbua na maanjumati mengine pale unapotoa order. Na yeye akiwa na muda wakufanya hivyo baada ya kazi zake za kila siku. Wanajumuiya wanamtakia safari njema na afya njema huko aendako. Picha kwa hisani ya Sophia, na Ny Ebra wa New York City.
No comments:
Post a Comment