ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 1, 2011

WANANCHI WAFAIDIKA NA HUDUMA ZA BURE ZA MATIBABU YA AFYA KATIKA MAONESHO YA MIAKA 50 YA UHURU YA UTOAJI HUDUMZA ZA AFYA TANZANIA.

 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiingia katika eneo kunakotolewa huduma mbali mbali za upimaji wa afya na  matibabu katika mabanda ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yaliyopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru katika utoaji huduma za afya Tanzania.

 Moja wapo ya bango lililopo katika eneo la kuingilia katika mabanda yanayotoa huduma hizo likionyesha huduma zinazotolewa bure kwa watu wote kwa kipindi chote cha maadhimisho hayo.
 Dkt. Rajabu Bushiri kutoka hospitali ya Amana ya Jijini Dar es Salaam katika banda la Kitengo cha Kupima Kisukari na Shinikizo la Damu akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo juu ya viashirio vya kupatwa na magonjwa hayo na njia mbali mbali za kuepukana nayo.
 Afisa Muuguzi Sista Zania Ndimbo kutoka Hospitali ya Amana akitoa huduma kwa mmoja wa watu waliojitokeza kupima ugonjwa wa Kisukari.
 Muuguzi Asma Msimbe akichukua vipimo vya damu kwa ajili ya kupima Ugonjwa wa Kisukari kwa mmoja watu waliojitokeza kupima Afya zao
 Bw. Shanmukeswar (Shanu) Kutoka kampuni ya kutengeneza dawa ya Sun Pharmaceuticals ya nchini India ambao ndio wadhamini waliowezesha kufanyika kwa  huduma ya bure ya vipimo vya Kisukari na Shinikizo la damu.
 Lucas Chagula kutoka Bohari Kuu ya Dawa Tanzania akitoa dawa kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la bohari hiyo baada ya kupima Afya zao. 
 Wafanyakazi wa Banda la Bohari Kuu ya Dawa kutoka kushoto ni Rehema Shelukindo, Lucas Chagula, Terry Edward na Gendi Machumani wakiwa wamekaa imara kabisa kutoa huduma kwa wananchi.
 Katika Banda la Ushauri Nasaha na Upimaji VVU lililopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Muuguzi Mshauri Rehema Kessy akitoa maelekezo sahihi ya jinsi ya kutumia mipira ya kiume Kondom kwa kijana  Frank Christopher.
 Banda la Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nalo halijabaki nyuma katika kutoa huduma bila malipo kwa wananchi wanaotembelea maadhimisho yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni Shamra shamra za kusheherekea miaka 50 ya  Uhuru ya Utoaji Huduma za Afya Tanzania. Pichani ni Dkt Fidelis Mgohamwende akichukua vipimo vya damu kwa mmoja wa wananchi.(Picha na zote na mo blog)
Kwa picha zaidi na maelezo Bofya Read More

 Katika siku ya pili ya maadhimisho ya utoaji huduma za Afya Tanzania tangu Uhuru Wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Kitengo cha Uchunguzi wa Awali wa Saratani ya Kizazi Wauguzi Maria Haule (kulia) na Genoveva Mlawa wakitoa huduma na maelezo mbalimbali kwa mmoja wa kinamama aliyejitokeza kuchunguza Afya yake.
 Dkt. Neema Ijani na Dkt. Jennifer Raymond wakiongea na binti aliyefika katika banda la Uchunguzi wa Saratani ya Matiti kuchunguza Afya yake.
 Baadhi ya wananchi wakisubiri katika foleni ya kupata huduma ya Bure ya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya Matiti kwa kina Mama.
 Afisa Mdhibiti Ubora kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Winfrida Mrema (kulia) akimfanyia vipimo mwananchi aliyefika katika banda hilo kwa ajili ya kujua afya yake.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika foleni katika banda linalotoa huduma ya Upimaji na Mtibabu ya Macho bure. 
  Kushoto ni Cardiac Nurse Angella Zakayo Msuya kutoka kitengo cha Magonjwa ya Moyo cha Hospitali ya Muhimbili akisikiliza maelezo ya Ally Mrisho mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam aliyefika katika banda hilo.
 Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge kutoka Kitengo cha Magonjwa ya Moyo akimhudumia Doris Peter.
 Wananchi wakimiminika katika banda linalotoa huduma za Upimaji wa FIGO Bure kwa ajili ya kujua Afya zao.
 ANGAZA nao hawakuwa nyuma katika utoaji huduma za kupima VVU na Ushauri  kwa usiri zaidi.
 Bendi ya Mjomba ikitoa burudani katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo wananchi wanapata Ujumbe kupitia muziki huo na burudani pia huku Upimaji wa Afya zao bure ukiendelea.
  Kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya mwaka huu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekweka banda la kitengo cha Magonjwa ya Ngono na Ngozi kinachotoa huduma bure ya Upimaji, Matibabu na  Ushauri kwa wananchi wanaotembelea maonyesho hayo ikiwa ni kuonyesha zaidi kuwajali Watanzania. Pichani ni Dkt. Benedict Bigawa akimhudumia mzee Abedi Maganga.
 Dkt. Jamil Kajuna wa Kitengo cha Magonjwa ya Ngono na Ngozi akimsikiliza mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam aliyetembelea banda hilo kupata huduma.
 Wananchi wakisubiri kupata huduma katika Banda la Magonjwa ya Ngozi na Ngono.
 Naibu Meneja Mpango kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi Dkt. Robert Joiah naye akifafanua huduma zinazotolewa katika banda hilo kwa wananchi waliotembelea maonyesho hayo. Wa pili Kulia ni Mshauri wa Kiufundi wa JICA/NACP Nobuhiro Kadoi.
 Muelimishaji Jamii kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) James Ndege akitoa maelezo kwa mwananchi aliyefika katika banda la Mamlaka hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka 50  ya Uhuru ya utoaji huduma za Afya Tanzania yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Katikati ni Mkurugenzi Usalama wa Chakula wa Mamlaka hiyo Bw. Raymond Wigenge.

No comments: