ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 4, 2011

MPANGO WA KUSTAAFU WA 401(K) KWA WATANZANIA WANAOISHI MAREKANI

401 (k) ni aina ya mpango wa kustaafu ambao unaruhusu wafanyakazi kuokoa pesa na kuwekeza kwa ajili ya kustaafu . Kwa njia ya 401 (k), unaweza kuidhinisha mwajiri wako kuhifadhi kiasi fulani cha fedha kutoka kwenye malipo yako kabla ya kodi ya mshahara wako, na kuwekeza katika mpango wa 401 (k). Pesa yako itahifadhiwa kwenye investments tofauti ambazo mwajiri wako anazitoa. Hakikisha kuwa kama mwajiri wako analinganisha kwa mfano 5%, ni lazima na wewe uweke 5%, kwani hii ni hela ya bure anakupa- Usiachie hizi pesa hatasiku moja ni za buree.

Wewe mwenyewe unaamua ni kiasi gani cha fedha(%), unataka kitolewe kutoka katika malipo yako kila pay cheki mpaka kufikia kiwango cha mwisho kilichowekwa na Internal Revenue Services (IRS). Kwa hivi sasa kiwango hicho ni $16,500(Mke na Mume ni $33,000). Kwa maana hiyo unaweza kuweka hizi hela pembeni bila kukatwa kodi kila mwaka.

Pia kwa maana hii , utapunguza kodi unayolipa kwani watakuwa wanakata kodi baada kutoa mawekezaji ya 401(k)  . Ina maana kwamba hela unazoweka pembeni kwa ajili ya 401(k) hulipi kodi, na pili zile zulizobaki unalipa kiasi kidogo cha kodi kwani umezipunguza kwa kuziweka kwenye 401(k)  . Kwa mfano, kama wewe Hulipwa $ 1000 kila malipo, na wewe kuchangia, sema 5% ($ 50), wewe utalipia kodi $ 950 tu. Hudaiwi kodi mpaka hapo utakapoamua kuchukua hela zako utakapostaafu ambapo wakati huo kipato chako kitakuwa kidogo na rate yako ya kodi itakuwa ndogo sana.

Akaunti ya akiba ya kawaida (saving account) au money market hairuhusu wewe kutokulipa kodi ya interest ya kila mwaka, inabidi ulipe. Hivyo katika akaunti ya akiba ya kawaida, ni kwamba wewe  unaweka pesa zako ambazo ushalipia kodi  na kila mwaka unalipa kodi kwa interest(riba) unayoipata kwenye akiba hiyo. Mpango huu mzima wa 41K unakusaidi na kukuokolea pesa .

Kumbuka, hata hivyo, kuwa kuwekeza katika mpango wa kustaafu wa kampuni yako ni sehemu tu ya mpango madhubuti wa kukusaidia utakapo staafu. Bado ni muhimu kuwa na akiba yako binafsi (Saving account) mbali ya Mfuko huu wa 401(k).


Itaendelea wiki ijayo.

Wenu

Iddi Sandaly
Mbezi@yahoo.com

1 comment:

Anonymous said...

MMH KUNAKURUDI NYUMBANI KWELI!