Beki wa Kili Stars, Shomari Kapombe (kushoto) akiwania mpira na Donald Ngoma wa Zimbabwe wakati wa mchezo wa Kombe la Chalenji Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Zimbabwe ilishinda mabao 2-1. (Picha na Yusuf Badi).
UWANJANI timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imefungwa mabao 2-1 na Zimbabwe, lakini imefuzu hatua ya robo fainali kutokana kanuni zilizowekwa kwenye mashindano ya Chalenji mwaka huu.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa mwisho jana Kundi A kwenye michuano hiyo kati ya Stars na Zimbabwe uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
wageni kuibuka na ushindi huo.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa mwisho jana Kundi A kwenye michuano hiyo kati ya Stars na Zimbabwe uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
wageni kuibuka na ushindi huo.
Michuano ya Chalenji mwaka huu inashirikisha timu 12 zilizogawanywa kwenye makundi matatu na kulingana na kanuni za Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa)
linalosimamia mashindano hayo, timu mbili za juu kutoka kila kundi zitacheza robo fainali.
Timu nyingine mbili ambazozitafanya idadi ya timu nane kwenye robo fainali, zitapatikana kwa mfumo wa zile zitakazokuwa na uwiano mzuri wa pointi, lakini hazikushika nafasi mbili za
juu kwenye kundi husika.
Kutokana na mazingira hayo, Kundi A ambalo Stars imo timu iliyoshika nafasi ya kwanza ni Rwanda yenye pointi tisa, ikifuatiwa na Zimbabwe yenye pointi sita, huku Stars ikiwa ya tatu ikiwa na pointi tatu na Djibouti ya mwisho haina pointi.
Kwa upande wa Kundi B timu zilizoshika nafasi mbili za juu ni Burundi yenye pointi saba na Uganda yenye pointi sita huku Zanzibar ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne na Somalia ya mwisho haina pointi.
Kundi C Malawi imeongoza ikiwa na pointi tano sawa na Sudan ambayo jana iliifunga Kenya bao 1-0 lakini Malawi ina uwiano mzuri wa mabao, huku Kenya ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu na Ethiopia ni ya mwisho ikiwa na pointi mbili.
Kulingana na kanuni za Cecafa, baada ya kupata timu hizo mbili za juu kwa kila kundi, timu ya kwanza kupenya kupitia kapu au kuingia robo fainali kwa kutumia mlango wa uani ni Zanzibar yenye pointi nne, kisha Kilimanjaro Stars nayo imefuzu kutokana na kuwa na pointi tatu nayo pia imepitia mlango wa uani kufuzu.
Kilimanjaro Stars na Kenya zinalingana pointi, lakini Stars ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, ambapo imefungwa mabao matatu na kufunga manne, hivyo ina faida ya
bao moja, wakati Kenya imefungwa mabao matatu na imefungwa mawili, ina deni la bao moja.
Kutokana na hali hiyo Stars itacheza robo fainali Jumanne na mshindi wa kwanza Kundi C ambaye ni Malawi, huku baadaye siku hiyo Zimbabwe iliyoshika nafasi ya pili Kundi B ikicheza
na Uganda.
Robo fainali nyingine itachezwa kesho, ambapo Zanzibar itaivaa Rwanda, huku Burundi
ikiikabili Sudan. Mechi zote zitakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa jana wa Stars, mabao ya washindi yalifungwa dakika 15 za kwanza, ambapo
bao la kwanza lilifungwa dakika ya kwanza na Donald Ngoma baada ya kutokea piganikupige
langoni.
Bao la pili lilifungwa dakika ya 11 na Leonard Fiyado baada ya beki Ibrahim Mwaipopo kumbabatiza na mpira kwenye harakati za kuokoa.
Ikicheza huku ikizomewa na baadhi ya mashabiki, Stars ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 85 mfungaji Mwinyi Kazimoto kwa mkwaju wa penalti, baada ya Mrisho Ngassa kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Habari Leo
No comments:
Post a Comment