ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 19, 2012

Anaswa na umeme akiangalia taarabu, afa-Habari Leo

MWANAFUNZI wa darasa la saba na mkazi wa Bungoni, Joseph Felix (14), amekufa papo hapo baada ya kunaswa na umeme wakati akiangalia muziki wa taarabu, mtaani kwao. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema kuwa mwanafunzi huyo alinaswa 
juzi saa 1.00 usiku katika maeneo ya Bungoni Ilala. 

Alisema kuwa wakati mwanafunzi huyo akiwa mtaani kwao akiangalia taarabu ghafla aliangukiwa na waya wa umeme na kunaswa hatimaye kufariki dunia papo hapo. 

Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana na upelelezi unaendelea. Wakati huo huo mwendesha pikipiki Isaka Halifa (23), mkazi wa Mwananyamala amekufa papo hapo baada ya pikipiki aliyokuwa akiiendesha kugongwa na gari. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 2.00 usiku katika barabara ya Morogoro eneo la Bahama na kuhusisha gari lisilofahamika likiendeshwa na dereva asiyejulikana. 

Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea 
kulisaka gari na dereva aliyehusika katika ajali hiyo ambaye alikimbia mara baada ya tukio hilo.

No comments: