ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 12, 2012

MAELFU WAJITOKEZA KUMPOKEA PROF LIPUMBA AKITOKEA MAREKANI

Maelfu ya wanachama na wafuasi wa CUF wakiwa uwanjani kumpokea Prof. Lipumba.
…Wakizunguka uwanja wa ndege wakiimba nyimbo za kumsifu Lipumba.
Gari lililojaa wafuasi wa CUF likiwasili uwanja wa ndege.
Wapenzi wa chama hicho wakimsubiri mwenyekiti wao.
Baadhi ya wawakilishi na wabunge wa CUF wakimsubiri Lipumba.
Waziri wa Afya wa serikali ya kitaifa Zanzibar,  Juma Duni Haji (kulia)akisalimiana na Mwawakilishi wa chama hicho.
Afande Sele (Kushoto) akitoa burudani katika mapokezi hayo.
Magari yakipita kwa taabu katika Uwanja huo.
Prof Lipumba akitoka ndani ya Uwanja wa ndege huku akiwapungia mikono wafuasi wa chama hicho.
..Akionyesha furaha yake kwa mapokezi hayo.
...Wapenzi wa CUF wakitaka kumvisha ya maua.
Prof akivishwa maua.
MWENYEKITI  wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim  Lipumba, amewasili jana akitokea nchini Merekani na kupata mapokezi ya kihistoria

Prof Lipumba alikuwa akirejea kutoka Marekani ambako alienda kujadili hali ya uchumi duniani.  Maelfu ya wanachama na wakereketwa wa chama hicho walijitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo waliyafunika karibu maeneo yote ya uwanja huo kwa ndani na nje.

                                  PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY, GPL

No comments: