MKAZI wa Mtaa wa Jamhuri katika Manispaa ya Lindi, Lucy Cassian (22), anatuhumiwa kumpa mtoto wake Richard Said (miezi minane) dawa ya kusafishia vidonda kwa kumnywesha ili afe kwa nia ya kupewa Sh 15,000 na mumewe ili afanyie biashara.
Kaimu Mganga Mkuu Mfawidhi, Dk. Edgar Mlawa alithibitisha kumpokea mama na mtoto wake aliyepewa dawa ya kusafishia vidonda, amelazwa katika wadi ya watoto katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine mjini hapa.
Mama huyo wa mtoto alisema alimwomba fedha mumewe, Said Richard, lakini badala yake, mume huyo anadaiwa kumshawishi amuue mtoto huyo ili amkopeshe 15,000 kwa nia ya kumsaidia kufanyia biashara.
Alidai mumewe huyo alishawahi kusema kuwa huyo mtoto siyo wa kwake.
Alisema hapo awali alimpa Sh 1,000 ambazo Sh 500 anunue sabuni na Sh 500 atumie kwa kunywa chai na kuamua kuondoka kwenda kwa mwanamke mwingine aliyezaa naye anayeishi Mnazi Mmoja.
Alisema ilipofika saa nane mchana, aliamua kuitoa dawa hiyo na kumnywesha mtoto, na haikuchukua muda, alifika mwanamke aliyemtaja kwa jina la Mama Shabani na kumwokoa kwa kumtafutia maziwa yaliyochanganywa na chumvi na hatimaye alipona na kumkimbiza hospitalini.
No comments:
Post a Comment