Ndugu zangu Watanzania DMV kwanza napenda kuwapongeza sana kwa kujitokeza kwa wingi katika upigaji kura Jumapili ya April 15, 2012 kusema ukweli ni jambo la kujivunia na kujipongeza sana kwamba DMV sasa inaelewa maana ya kuwa na Jumuiya yetu.
Kama alivyosema mwenyekiti wa marekebisho ya katiba siku ya uchaguzi kwamba uchaguzi sasa umeisha na angependelea kuona upendo unarejea miongoni mwetu turudishe umoja wetu kama Mtanzania, tumezaliwa Tanzania, dini yetu Tanzania, Tunaipenda Tanzania kwani wewe ni Mtanzania.
Ni jambo linaloshangaza kuona uchaguzi umekwisha bado malumbano ya chuki yanaendelea kupitia comments za Vijimambo kusema ukweli ni jambo la aibu sana kwa WanaDMV, sisi tunatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kama tulivyofanya kwenye uchaguzi Jumapili, kuweka Historia kujitokeza kwa wingi kama tulivyoweka Historia ya kuwa Jumuiya ya kwanza kuanzishwa hapa Marekani tuna kila sababu wa kuwa hivyo hapa ndio makao makuu ya Serikali pia ndio Ubalozi wetu ulipo.
Kwa maana hiyo basi naomba tuchangie mawazo ya jinsi gani ya kuendeleza na kuboresha Jumuiya yetu, Jumuiya haina pesa ni mipango gani Jumuiya inaweza kufanya iliijitegemee au kujiongezea kipato, nini kifanywe kurudisha mshikamano na ukaribu wa wanajumuiya, una ushauri gani kuhusiana na Jumuiya iwe na Website yake kwa lengo la kua karibu na wanajumuiya wake na mengine mengi.
Tafadhali naomba unavyonichekea na kunichangamkia kwa upendo unaponiona naomba iwe hivyo pia unapoandika Comment kwenye Vijimambo, Asante, Mungu ibariki Jumuiya yetu, Mungu ibariki DMV.
6 comments:
JAMANI TUPENDANE
watu wanaoleta chuki wanatakiwa wakanywe siyo kuwaachia tu. for years DMV (and ex-DMVs) imekuwa na watu wenye chucki binafsi na kutukanana na wenyewe wanaita freedom of speech and nobody says anything to them. seriously, hii tabia inatakiwa ifikie upeo. mie kama member wa kudumu hawa watu siwafagilii kabisa na nikikutana nao nakaa nao mbali nawaogopa kama ukoma!. seriously, this needs to STOP!
Mpwa,
Ni kweli hii ni blog yetu tunaipenda inayotupa habari mbalimbali, blog hii sio posta ya kupostia chuki zako humu. comments zako zikiwa za heshima zitaandikwa, ila sio mahali pa kujibizana chuki zenu humu. kama una chuki na mtu, na wewe unajiamini onesha uanamke/uanaume wako mwendee face to face. Hebu tukue kimwili, kiakili na kitabia.
Mdau mkuu wa vijimambo
Kaka Luka mimi naomba ni-ignore hili swala la chuki hapa DMV, maana tukiendele kulizungumzia halitoisha. Lets kill all that chuki with kindness and zero room for drama etc. Ushauri wangu…Jumuiya iwe na website yake; kwasasa hivi sababu Jumuiya haina pesa basi waanzishe tu ka blog ambacho baadaye kanaweza kuhamishiwa kwenye website. Hiyo blog/website kuwe na news, info mbalimbali za kuweza kutusaidia sisi wana jumuiya kwa jambo moja ama lingine, pia inaweza kutangaza matangazo mbalimblai kama babysitters/mafundi/wapishi/wanasheria/madaktari etc in return hao wanaotangaziwa biashara zao walipe jumuiya pasenti fulani kutoka kwenye hayo mapato ya wao kutangaziwa biashara, hilo ni moja. Kingine wanazeza pia kuweka info za vitu kama health/dental/life/car insurance, paydayloans, na kuchaji asilimia kidogo tuu pale mtu anapotumia jumuiya kuapply….idea ni ziko nyingi sana, ili ideas zitikilizwe kwa mpango ingekuwa muhimu na rahisi kama kungeteuliwa kikundi kidogo tu(au hata watu wawili watatu) kuzisimamamia hizi ideas na baadaye zijadiliwe na
uongozi na baada ya hapo wanajumuiya wajulishwe…Mimi niko tayari kujitolea kusaidia kwenye hili and I can commit 3hrs daily. Ahsante Kaka Luka...
Asante sana Luke kwa ujumbe wako na umefika,kwanza nimefurahi ulivyosema hapo sentensi ya mwisho Tafadhali naomba unichekee na kunichangamkia........(malizia)hiyo kweli naikiubali mtu anakuchekea lakini kumbe rohoni mwake hayuko hivyo!huo ni unafiki mkubwa na DMV tunao huo.Watanzania tuna upendo nakuoneana huruma,lakini hilo hapa dc naona limetoweka,hakuna upendo kabisa.Uchaguzi umekwisha salama tunaomba utulivu,kuna baadhi ya watu wanajisifu kabisa kuwa natukana na hakuna mtu yeyote atakae nifanya lolote,tafakari binadamu wewe!wewe ni nani?haujaamuliwa tu au watu wamekupuuza!.Tuangalieni mbele.Ushabiki haufai!unawaharibia akina dada hapa,na wengine hamuishi kwenye mji huu lakini mnaleta fitna!kwanini msiwe kwenye jumuiya yenu?inaelekea huku mliko hamthaminiwi sasa mnataka kujipendekeza DMV na huku sasa pia hatuwataki wala hatuwatambui.
Luke inaelekea ungekua huapruvu comments watu wangechinjana hapa,naamini hua unapokea vigongo kweli,lakini ndio inatakiwa muandishi awe na siri na ninaamini una siri nyingi sana lakini unajua kutunza mno,kazi nzuri sana mpwa,endeleza vijimambo.
Ahsante sana mpwa kwa maneno mazuri uliyoyaandika kwani umeonyesha upendo lakini hapa DMV kabla hawajauonesha upendo kwanza waondoe CHUKI ZAO BINAFSI.
Post a Comment