ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 20, 2012

Waziri Magufuli atoka hospitali




Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ambaye alilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, baada ya kuugua ugonjwa wa shinikizo la damu (BP), ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya afya yake kutengamaa.

Akizungumza na NIPASHE, Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainabu Chaula, alisema Magufuli ambaye alipokelewa juzi saa 2.10 asubuhi hosptalini hapo aliruhusiwa jana mchana baada ya afya yake kutengemaa.

Awali, Dk. Chaula alieleza gazeti hili kuwa Magufuli alifika hospitalini hapo mara baada ya kusikia maumivu ya kichwa wakati akijiandaa kwenda kuhudhuria vikao vya Bunge.



“Tumegundua kuwa anasumbuliwa na presha na tumeanza kumpatia matibabu. Sasa anaendelea vizuri maana presha yake iko normal (ya kawaida) na tusingeweza kumruhusu wakati ule kwa sababu angerejea nyumbani atakosa uangalizi wa kitaalam,” alisema Dk. Chaula ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya ndani katika hospitali hiyo.
Dk. Chaula alisema Magufuli alilazwa katika Chumba cha Wagonjwa wanao (ICU) ili aweze kupata uangalizi wa karibu zaidi wa wataalam.
Hata hivyo, alisema katika jitihada za kumpa muda wa kumpumzika zaidi, wamelazimika kuweka mlinzi mlangoni ili kuzuia watu kuingia.
Alisema waliomtembelea na kupewa ruhusa ya kumuona ni Katibu wake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
CHANZO: NIPASHE

No comments: