TANZANIA COMMUNITY LEADERS ASSOCIATIONS
Kwa Wanajumuiya Watanzania Marekani
Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Watanzania, imo katika mchakato wa marejeo ya katiba ya nchi. Ni makusudio yetu kuishirikisha jamii yetu ya Watanzania Marekani katika mpito huu wa kihistoria. Isitoshe, kuna mahitajio ya kikatiba yanayoigusa jamii ya Watanzania Marekani.
Hivyo basi; TCLA inapenda kuwajulisha nyote juu ya zoezi la ukusanyaji wa mapendekezo ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, linalosimamiwa na chombo hiki. Tunashauri kila mtanzania kuirejea katiba ya Tanzania kwa makini na atume mapendekezo yake kwa uongozi wa TCLA kwa kupitia barua pepe ifuatayo: katiba@tcla-usa.org
Tafadhali andika mapendekezo yako katika utaratibu ufuatao: Andika namba ya kifungu/vifungu unacho/(vyo) ki/(vi)kusudia, nukuu ki/(vi)pengele cha/vya zamani na andika pe/(ma)ndekezo ya/(vya) ki/(vi)fungu ki/(vi)pya. Ukipenda unaweza ambatanisha jina lako kamili na mji unaoishi (sio lazima).
Mwisho wa upokeaji mapendekezo ya katiba ni June 23.
Kwa niaba ya TCLA, natanguliza shukrani kwa jitihada na ushirikiano wenu katika kuimarisha umoja wa kijamii na maendeleo ya nchi yetu.
NB: link ya katiba ni ya Tanzania ni:
Nassor Ally, Chairman
TCLA-US
P. O. Box 52531
Durham, NC 27717
"If a door is shut, attempts should be made to open it; ......... at the expense of those inside."Julius Kambarage Nyerere.
No comments:
Post a Comment