Sakata la nani alifaidika na fedha ya rushwa iliyoambatana na yale mauzo ya ile rada ya ‘bei mbaya’ iliyouzwa kwa Tanzania na Kampuni ya kimataifa ya vifaa vya ulinzi, usalama na anga ya Uingereza (BAE Systems), imewekwa hadharani na Kanali Mstaafu Andrew Feinstein wa Jeshi la Marekani katika kitabu chake cha ‘The Shadow World, Inside the Global Arms Trade’.
Kanali Feistein katika kitabu chake hicho mbali na kuzungumzia namna rushwa ilivyotawala katika mauzo ya silaha duniani, amewataja kwa majina watu walioshiriki kufanikisha biashara haramu ya uuzaji wa rada pamoja na makampuni na benki walizozitumia kufanikisha shughuli hiyo nzima.
Alisema makampuni yaliyoshiriki kufanikisha mauzo hayo kwa Tanzania ni ile ya BAE Systems yenyewe pamoja na kampuni yake tanzu iitwayo BAE’s Red Diamond Trading Ltd na kampuni ya Envers Trading Corporation ambayo ilisajiliwa Panama na ndiyo iliyochukua nafasi ya kisiri kama mshauri wa BAE Systems.
Kanali Feistein anaendelea kuyataja makampuni mengine kuwa ni kampuni ya Merlin International Limited ya Tanzania ambayo ilimilikiwa na washirika wawili wa kibiashara Sailesh Vithlani na Tanil Somaiya, ambao walikuwa mawakala wa BAE System waliofanikisha mauzo ya rada hiyo.
Kampuni nyingine kwa mujibu wa kitabu hicho ziliyoshiriki kwenye biashara hiyo, ni Franton Investment Limited inayomilikiwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mbunge wa sasa wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
Kampuni ya Chenge ndiyo iliyotumiwa na BAE System kumuingizia dola za Marekani milioni 1.5.
Kampuni nyingine iliyotajwa na Kanali Feistein katika kitabu chake hicho ni ya Langlay Investment Limited inayomilikiwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Idrissa Rashid na ambayo ilitumiwa na kampuni ya Franton Investment Limited ya Chenge kuingiza dola za Marekani 600,000.
Kanali Feistein anawataja mawakala wa BAE Vithlani na Tanil kuwa ndiyo vinara walioshiriki kufanya mazungumzo na kufaulu kuishawishi serikali ikakubali kununua rada hiyo pamoja na upinzani toka kwa baadhi ya mawaziri wa serikali ya Uingreza na wadau mbalimbali wa kimataifa kama Benki ya Dunia.
Anasema katika biashara hiyo, mikataba miwili ilitengenezwa ambapo katika ule wa awali walitengewa asilimia moja kama kamisheni yao kutoka kwenye mauzo ya jumla ya rada, lakini vile vile ulitengenezwa mkataba mwingine haramu ambao ndiyo uliwapa kamisheni ya asilimia 30.
Anaeleza kwamba BAE System kwa kuzingatia mkataba wa pili ilitoa kiasi cha pauni za Uingereza milion 6.2 kwa akaunti ya Vithlani iliyoko Uswisi, fedha ambazo ndizo zinazoamika kuwa ziliingia katika mgawo.
Kwa upande wa Chenge, mchango wake kama ulivyoelezwa kwenye kitabu hicho ni kwamba alitoa ushauri wa kisheria kwa mujibu wa madaraka yake ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliokuwa nao wakati ule, kwamba biashara hiyo haikuwa inakiuka taratibu za msamaha wa madeni uliokuwa umetolewa kwa wakati huo kwa Tanzania.
Aidha, Kanali Feinstein katika kitabu chake anataja kuwa kampuni ya Franton Investment Limited iliyokuwa inamilikiwa na Chenge ilianzishwa makusudi kwa ajili ya kufanya kazi za kuingiziwa na kuhamisha fedha na ndiyo iliyotumiwa na BAE System kumuingizia kitita cha dola za Marekani milion 1.5 na vile vile kuhamisha dola 600,000 kutoka kwenye akaunti yake na kuzingiza kwenye akaunti ya Dk. Rashid kupitia kampuni yake ya Langlay Investment Limited.
Dk. Rashid anatajwa na Kanali Feinstein kwamba biashara ya rada ilifanyika wakati yeye akiwa ni Gavana wa BoT na ndiye hasa aliyeidhinisha mipango yote ya kifedha ya ununuzi wa rada hii, chini ya makubaliano kwamba dhahabu ya Tanzania iliyokuwa ikihifadhiwa BoT, iwekwe kama dhamana ya kupata mkopo kutoka Barclays.
Aidha, katika kitabu hicho Feistein anasema alikuwa ni Dk. Rashidi aliyekubali kwamba endapo yangetokea matatizo yoyote katika mkataba huo, basi sheria za Uingereza ndizo ambazo zingetumika kufikia suluhisho, badala ya zile za Tanzania.
Jana NIPASHE iliwatafuta Chenge na Dk. Rashidi ili wazungumzie habari za kitabu hicho, lakini simu zao zilikuwa hazipokelewi.
Uwepo wa habari za kitabu hiyo zinaibuka wakati kukiwa na mvutano ndani ya Bunge linaloendelea mjini Dodoma juu ya matumizi ya Sh. bilioni 72 zilizorejeshwa na BAE System kwa Tanzania kutokana na ufisadi wa rushwa ya rada hiyo.
Wabunge wa Zanzibar wamekuja juu wakitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) nayo ipewe mgawo wa fedha hizo kwa kuwa zilizotumika kununua rada zilikuwa ni za Muungano na ni haki yao nao kupewa mgawo.

CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Aibu, serekali na viongozi wake wakubwa na nafasi zao badala ya kusaidia nchi Yao, ufisadi unawazidi.
Post a Comment