Wananchi wakiwa na hamu ya kumuona Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka wakati gari lililombeba likiwa limesimama katika lango la kuingilia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo, tayari kusafirishwa kwenda India kutibiwa baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya. Picha zaidi uk. wa 3. (NA KAMANDA WA MATUKIOBLOG)
Wanaharakati wakiwa na mabango walipokwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo, kumsindikiza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka aliyekuwa anasafirishwa kwenda India kutibiwa baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya
Picha kwa hisani ya FULL SHANGWE
Picha kwa hisani ya FULL SHANGWE
3 comments:
mhh India anakimbia nini Muhimbili? hao wenzie waliolala wodini sio wagonjwa? mgonjwa mmoja anatumia pesa India ya kutibu wodi nzima huu ni uzalendo anaogomea Dk.Ulimboko kama kweli wewe ni kiongozi wa mgomo atibiwe muhimbili mpaka apone vinginevyo hatuna imani nae tena sio mwanaharakati mwenzetu na wewe ni sawa na hao vigogo wenzako wote mnatibiwa India mnatufumba macho sisi walala hoi
doctor umetugeuka siamini unaenda india
angetibiwa vp wakati mgomo unaendelea muhimbili, pia yeye analili haki yake ili apate mazingira ya kazi yatakayomuwezesha kufanya kazi kwa umakini zaidi,na hiyo ni kwa manufaa ya watanzania ,sio yeye tu. hao viongozi wenu wamewafanyia nini cha maana?
Post a Comment