KAMANDA KOVA AZUNGUMZIA TUKIO LA KUTEKWA DR ULIMBOKA
Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye
hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa
msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na
kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu
alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
5 comments:
Dr. Steve Watanzania wanajua harakati zako katika kudai haki na hali bora ya Madaktari nchini kaza buti Mungu atakujalia ku-recover soon na haki zitapataika dhidi ya ufisadi na udhalimu wa serikali ya Kikwete iliyojaa wababaishaji
Kamanda Kova acha kuwazuga Wabongo. Wabongo wamechoshwa na usanii wa serikali ya Kikwete. Sasa unaunda tume ya kuchungu za nini wakati inajulikana fika kuwa Dr. Ulimboka amefanyiziwa na Usalama wa Taifa kwa kuwa ngangari katika kudai haki na hali bora za Madaktrai nchini Tanzania. Serikali imeshindwa kumrubuni sasa inatunmia vitisho ili Dr. Ulimboka atangaze mgomo basi. Ni nanio asiyek=jua kuwa sekali imemrubuni kwa mamilioni na post mbalimbali asitishe mgomo lakini jamaa akatolea nje offer zenu sasa mnataka kumuua. Serikali hii inafikiri kila mtu ni fisadi tu! Big up Dr Ulimboka usiogope vitisho kuwa ngangari tu mpka haki zenu zipatikane.
Walichofanya kwa Dr. Ulimboka ni unyama. Waliofanya kitendo hicho ni wanafiki, wapungufu wa mawazo na fikra za kisomi. Kama hawapendi sababu za mgomo, kwa nini wasitumie nguvu ya hoja kuwasilisha mawazo yao? Mungu ambariki Dr. Uli apone aendelee na kazi yake ya kutetea uboreshaji wa kazi na fidia kwa waganga.
huyu doctor kapanga na wenzake kwa vile wameona serikali hawapatilizi madia yao acheni zenu jamani hizo yeye ndo msanii na siyo serikali
Sawasawa. wanaomia ni wanyonge wakati madaktari wamegoma... matajiri wanakwenda private, wamkungute sawasawa na amerudishwa hukohuko muhimbili walikogoma .. wampe dawa ya moto wake..
Post a Comment