Amiri wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid
--
Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya
Kiislamu (JUMIKI) imepinga uvumi uliosambazwa nchini kuwa jana kungekua
na maandamano ya Jumuiya hiyo na kudai kuwa propaganda hizo zinaendeshwa
na baadhi ya watendaji katika jeshi la polisi na usalama wa taifa ambao
hawaitakii mema Jumuiya yao.
Kiislamu (JUMIKI) imepinga uvumi uliosambazwa nchini kuwa jana kungekua
na maandamano ya Jumuiya hiyo na kudai kuwa propaganda hizo zinaendeshwa
na baadhi ya watendaji katika jeshi la polisi na usalama wa taifa ambao
hawaitakii mema Jumuiya yao.
Hayo yamesemwa na Amiri wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid Ahmed wakati
alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari
Maelezo Zanzíbar kuhusiana na tuhuma ambazo wamezitoa kwa Jeshi la
Polisi dhidi ya Jumuiya yao.
Amedai kuwa Jumuiya haijapanga maandamano kwani ni taasisi inayofanya
kazi zake kisheria nakwamba hata ikitokezea kufanya maandamano basi
watafuata taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kulitaarifu rasmi
Jeshi la Polisi.
Aidha amedai kuwa kuna mkakati wa muda mrefu wa kutaka kuwabatiza
viongozi wakuu wa jumuiya hiyo kesi za ugaidi hususan Amir Mkuu wa
jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed ili kuzima vuguvugu
la kudai Zanzibar huru.
Shekh Faridi amedai kuwa inasemekana kuna mahusiano makubwa baina ya
watendaji ndani ya Jeshi la polisi pamoja na baadhi ya wageni
wanaosadikiwa kuwa ni raia wa Marekani juu ya kuutekeleza mkakati huo
baada ya kuwa tayari umeshakamilika.
Amedai kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za kiraia ambao umekuwa
ukifanywa na Jeshi la Polisi Zanzibar kwa kuwanyima haki ya kufanya
mihadhara yao ndani ya Misikiti ambapo Juni 17 mwaka huu wananchi
mbalimbali walijeruhiwa kwa mabomu katika vijiji vya Donge,Mkwajuni na
Mahonda.
Ameliomba Jeshi la Polisi kufanya kazi zake za kulinda usalama wa
wananchi na mali zao na kuacha kufanya kinyume chake kwani huko ni
kuchochea chuki kati ya Jeshi hilo na raia.
Amesisitiza haja ya wazanzibari kuungana na kuachana na Itikadi zao za
kivyama katika kudai hadhi ya Rais na mamlaka ya Nchi ya Zanzibar ndani
na nje ya Zanzibar pale tume ya mabadiliko ya Katiba itakapoanza kazi
zake.
Kwa upande wake Naibu Naibu Amir Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya
Kiisilam Sheikh, Azan Khalid Hamdan amewaomba wanahabari nao kuwa makini
katika taaluma yao kwa kufanya usawa wa taarifa ambazo wamekuwa
wakizitoa.
Hivi karibuni Jumuiya hiyo ilitangaza rasmi kushiriki kikamilifu katika
zoezi zima la kutoa maoni yao katika mchakato wa kupata Katiba mpya ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kubadili msimamo wao wa awali wa
kuisusia Tume hiyo.
MWISHO.
IMETOLEWA NA
HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment