Mgonjwa akihamishwa kutoka Wodi ya Kibasila katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), iliyopo Dar es Salaam jana, ili kupelekwa katika
hospitali nyinyine kutokana na tihsio la kuwepo kwa mgomo wa madaktari,
katika hospitali hiyo na nyingine za serikali sehemu mbali mbali nchini
wanaodai stahiki zao mbali mbali, kwa madai ya serikali kushindwa
kuzitekeleza
MADAKTARI nchini wameanza mgomo katika baadhi ya hospitali nchini
baada ya Serikali kushindwa kutekeleza madai yao waliyowasilisha katika
Kamati ya Majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Mgomo
huo umetangazwa na Jumuiya ya Madaktari nchini huku ikifafanua kwamba
kati ya madai kumi waliyotaka yatekelezwe na Serikali, hakuna hata moja
lililofanyiwa kazi. Hata hivyo, jana madaktari hao ambao walikaa vikao
vya majadiliano na Serikali kwa siku 90 baada ya kusitisha mgomo wao wa
pili, wamesema katika madai yao kumi, hakuna hata moja lililotekelezwa
na Serikali. Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Stephen Ulimboka jana
aliwaeleza waandishi wa habari kwamba ili warejee kazini, Serikali
inatakiwa kutekeleza madai yao yote na kusisitiza kwamba dai lao la
kwanza ni kuitaka Serikali kuboresha huduma za msingi kwa wagonjwa.
“Mgomo
umeanza leo na hauna kikomo, lengo ni kuishinikiza Serikali kutekeleza
madai yetu, hata zile huduma za dharura nazo kuanzia kesho (leo)
zinaweza kusitishwa,” alisema Dk Ulimboka. Wakati Ulimboka akieleza
hayo, huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya
Mifupa (Moi) ilikuwa ikitolewa kwa kusuasua huku baadhi ya wafanyakazi
wakisisitiza kuwa mgomo huo upo.
No comments:
Post a Comment