Walusanga Ndaki
Katika mazingira ya kawaida nchini Tanzania, si vyema kutaja makabila ya watu lakini kwa ajili ya kumbukumbu kwa wale wasiofahamu ni kwamba Nsilo Swai alikuwa miongoni mwa mawaziri sita Waafrika waliounda baraza la mawaziri wakati Tanganyika inapata uhuru wake mwaka 1961.
Vilevile, Swai alikuwa Mchagga wa kwanza kuwa waziri katika baraza hilo lililokuwa chini ya Waziri Mkuu, Julius Kambarage Nyerere. Jambo hili ni moja ya mambo yaliyotokea miaka ipatayo 51 iliyopita.
Swai (kwa sasa marehemu), jina lake kamili ni Asanterabi Zephaniah Nsilo Swai, aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda, wakati huo akiwa na umri wa miaka 35 tu.
Swai (kwa sasa marehemu), jina lake kamili ni Asanterabi Zephaniah Nsilo Swai, aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda, wakati huo akiwa na umri wa miaka 35 tu.
Kwa kifupi, Swai (aliyekuwa akitaniwa na marafiki zake kama ‘Bwana Miwani’ kwa sababu ya kuvaa miwani muda wote), alipata elimu katika Vyuo Vikuu vya Makerere (Uganda), Bombay (India) na Pittsburg (Marekani) ambako alipata stashahada.
Aidha, mwanasiasa huyo alisoma Chuo Kikuu cha Delhi (India) ambako alipata shahada ya uchumi.
Mbali na wadhifa wa uwaziri, Swai alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uchumi na Starehe ya chama kilichokuwa kikitawala wakati huo cha Tanganyika African National Union (TANU).
Mbali na wadhifa wa uwaziri, Swai alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uchumi na Starehe ya chama kilichokuwa kikitawala wakati huo cha Tanganyika African National Union (TANU).
Kwa ufahamu zaidi, miongoni mwa watu watatu walioshinikiza Tanganyika ipate uhuru wake Desemba 9, 1961 na si Juni 1962 alikuwa ni marehemu Swai.
Awali, Uingereza ilipendekeza Tanganyika ipate uhuru Juni 1962, lakini kutokana na matatizo ya kiutawala, tarehe hiyo ikasogezwa hadi Desemba 9, 1962 jambo ambalo wawakilishi wa Tanganyika walilikataa na kurudishwa nyuma hadi Desemba 1961.
Sababu kuu ya Uingereza kusogeza mbele ilikuwa ni mwezi Juni taifa hilo husherehekea ‘bathidei’ ya Malkia Elizabeth wa Pili, hivyo asingeweza kuja Tanganyika kuwa mgeni wa heshima.
Katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo, Julius Nyerere alimteua Nsilo Swai, Oscar Kambona (marehemu) wakati huo akiwa Waziri wa Elimu na yeye mwenyewe. Walikutana na Waingereza na kuamua Tanganyika ipate uhuru Desemba 9, 1961.
Chanzo: GPL
No comments:
Post a Comment