ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 3, 2012

PICHA ZA RACE OF CURE ZA TEAM TANZANIA

Juu na chini ni Viatu vya Mr. TZ mwanamuziki wa kizazi kipya anaeishi DMV (DC, MD, VA) alivyotumia kwenye Race Of Cure.
 
 Kushoto ni Sophia Andrew akiwa na Joyce Kasembe wakati walipokuwa kwenye matembezi ya Susan G. Komen.
 Kushoto ni Aunty Zuhura akiwa na mnusurika wa Saratani ya matiti, Aunty Rehema.
 Team Tanzania wakipata picha ya pamoja.
 Baadhi ya Team Tanzania wakipata picha ya pamoja.
 Aminata akipata picha alipokua kwenye matembezi ya Susan G. Komen.
 Team Tanzania wakiwa na furaha kwenye matembezi hayo ya Susan G. Komen yaliyofanyikia Washington, DC June 2, 2012.
 Dr. Hamza Mwamoyo yeye na familia yake hushiriki kwenye matembezi haya kila mwaka.
Timu Tanzania ilipokua imekanyaga Finish Line ya Maili 3.2 sawa na kilomota 5 wakiwa na furaha.

WATANZANIA WASHIRIKI MATEMBEZI YA SUSAN G. KOMEN.

Washiriki waliojiandikisha upande wa Tanzania Mwaka huu wa 2012 walikuwa wachache tofauti na mwaka 2011, Watanzania waliojiandikisha Mwaka huu 2012 walifikia 24 hii ni idadi ndogo ukilinganisha na mwaka 2011 ambapo idadi ya Watanzania ilikuwa 54.

Lakini mwaka huu wa 2012 matembezi haya yamekua na mvuto kwa Watanzania wengi tofati na mwaka 2011 kwa maana ya kwamba Watanzania waliojiandikisha mwaka 2011 walikuwa 54 na waliojitokeza kwenye matembezi ni 30 tu.

Mwaka 2012 Watanzania waliojiandikisha walikuwa 24 na waliojitokeza kutembea walifikia 40 na hii inawezekana kutokana na kukosa muda iliyopelekea watu wengi washindwe kujiandikisha japo nia ilikuwepo.

Matembezi ya Susan G. Komen hufanyika kila mwaka na hushirikisha watu wa mataifa mbalimbali tukiwemo Tanzania. Susan Goodman Komen ni Mmarekani aliyefariki kwa Saratani ya Matiti, alizaliwa mwaka 1943 huko Peoria, Illinois, Nchini Marekani na aligundulika ana saratani ya matiti alipokua na miaka 33 na kufariki kwa ugonjwa huo alipokua na miaka 36.

Mwaka 1980 mdogo wake Susan G. Komen anayeitwa Nancy Goodman Brinker ambae alimuahidi dada yake kwamba atafanya kila linalowezekana kama si kuutokomeza kabisa ugonjwa huu basi kuupunguza kwa kiasi kikubwa kwa kuanzisha matembezi ya Saratani ya Matiti kwa ajili ya kuchangisha pesa zitakazosaidia kuelimisha Dunia kuhusu ugonjwa huu.

Kuanzia mwaka 1982, Nancy G. Brinker ameishachangisha $2 bilioni kwa ajili ya kusaidia research ya Saratani ya Matiti, waathirika kupata matibabu bure na mambo mengine mengi. Pia Susan G. Komen inashirikiana na Nchi zaidi ya 50 Duniani na ina Watu wanaojitolea zaidi ya 100,000.

No comments: