ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 29, 2012

USISUBIRI MPAKA AFIKIRIE KUTAFUTA WA KUMTULIZA!-2



HUU ni uwanja wa kujifunza na kuongeza maarifa kuhusu mapenzi. Ukiwa mdau wa ukurasa huu hutakuwa na cha kupoteza. Utakuwa unaongeza kila siku kitu kipya katika ubongo wako kuhusu uhusiano.
Suala la kuteseka kwenye mapenzi halitakuwa upande wako tena. Ndugu zangu, kujifunza ndiyo msingi wa kila kitu katika maisha. Hebu fungua ubongo wako upate kuingiza vitu vipya sasa.

Leo nahitimisha mada yetu ambayo ilianza wiki mbili zilizopita. Nazungumza kuhusu mawasiliano ya uhitaji wa faragha kwa wanandoa. Marafiki zangu, kama nilivyoeleza katika matoleo yaliyotangulia, faragha ni kati ya misingi ya ndoa.
Hata hivyo, tatizo linakuja ni wakati gani unahitaji na kufahamu kama mwenzako anahitaji tendo hilo. Ugumu umeonekana pale ambapo mwenzi wako anaweza kuwa amewaka kwa tamaa akikuhitaji, lakini ukashindwa kuelewa uhitaji huo.
Ukweli ni kwamba, kwa upande wa wanaume hawana tatizo hilo kabisa, maana wao ni waamuzi na maumbile yao hayana matayarisho makubwa.
Kama anamhitaji mwenzake, akirudi kazini ataoga, atakula na kwenda kulala. Yeye anaanzisha, mkewe hana ujanja labda awe na dharura muhimu. Tatizo lipo kwa wanawake ambao wengi huwa hawawezi kusema chochote.
Wiki iliyopita niliwaelezea wale machakaramu, ambao hawashindwi kuelewa wazi hisia zao moja kwa moja kuwa wanawahitaji wenzi wao. Wengine wanaweza kutuma meseji hata mchana wakieleza kwamba wanawahitaji wenzi wao siku hiyo.
Hata hivyo, niliweka angalizo kwa baadhi ya wanaume ambao hawapendi tabia hiyo. Si tu kwamba hawapendi bali huwapunguzia kujiamini katika tendo la ndoa. Hebu sasa leo tuingie katika hatua nyingine, tuone makundi yaliyosalia.

WANAOZUNGUMZA KWA VITENDO
Hawa si wakimya. Wanaweza kuwa wacheshi sana na wakali wa kuanzisha mada, lakini linapofika suala la faragha na yeye akawa anamuhitaji mwenzake, hana ujanja wa kufungua kinywa chake na kumweleza mumewe.
Lazima umtambue mwanamke wa aina hii. Kwa sababu hana uwezo wa kueleza anachohitaji, atatumia ishara kuonesha nia yake.
Kwanza ataonekana kuhitaji sana uwahi kurudi nyumbani. Kuanzia muda wa jioni atakusisitiza uwahi kurudi nyumbani.
Wengine huenda mbali zaidi na kusema kwamba ana mazungumzo muhimu au uwahi kurudi nyumbani. Cha kushangaza, hata unaporudi nyumbani, kunakuwa hakuna cha maana zaidi ya kukuambia: “Nimeku-miss dear, nilitaka uwe karibu yangu.”
Mavazi atakayokuwa amevaa nayo ni kielelezo tosha kwamba anakuhitaji. Utamkuta amevaa nguo nyepesi zinazoonesha umbile lake n.k
Wakati wa kuoga, hatakubali kwenda peke yake. Atakulazimisha muoge pamoja. Unapofika muda wa kupata chakula, pia atapenda zaidi mle pamoja kimahaba. Atatumia muda mwingi kukulisha na kutabasamu muda wote.
Alama nyingine ni kutaka muingie chumbani kulala mapema. Unaweza kushangaa baada ya kuingia chumbani akalala kimya, kama vile hana habari na wewe. Si kweli, hapo ameshamaliza kazi yake, anakusubiri wewe!
Hapo mwanaume unapaswa kumjua mwanamke wako na kuhakikisha anapata kile anachokitarajia. Marafiki zangu, ni rahisi sana kwa mwanaume kutuliza maruhani yake hata kama alikuwa akitaka na akakosa kuliko mwanamke ambaye anatamani kufurahia na mume wake halafu akakosa!
Ni fahari sana mwanamke kupata haki yake pale anapoonekana kuhitaji zaidi. Wanaume wana uwezo mkubwa wa kustahimili hali hiyo kuliko wanawake.
Onesha uanaume wako pale mwenzi wako anapokuhitaji, vinginevyo ni wazi kwamba utakuwa unamfanya mwenzako afikirie vinginevyo!
WAKIMYA
Hawa ni wale ambao hawawezi kusema chochote wala kuonesha alama za kuhitaji. Jambo kubwa kwako kwa mwanamke wa namna hii ni kusoma mahali hisia zake zilipo. Unapokuwa naye faragha hakikisha unajua himaya yake ipo wazi.
Ukijua ni rahisi sana; hata kama anaonekana mkimya, jaribu kumgusa sehemu ambayo unaamini huwa inamwongezea msisimko. Kama yupo tayari utajua tu na kama ni vinginevyo pia utafahamu!
USIKARIBISHE USALITI
Kwa kuyasoma yote hayo na kuyaelewa kisha kuyafanyia kazi ni wazi kwamba ndoa yako itakuwa salama. Ndugu zangu wakati mwingine wapenzi wetu wanatusaliti kwa kutaka wenyewe. Bila shaka kuna kitu umejifunza.
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na Who is Your Valentine vilivyopo mitaani.

2 comments:

Anonymous said...

Asante mwandishi! maana saa nyingine unakuta umezidiwa na upo kitandani ukijigalagaza.....lkn jamaa unakuta hata haelewi! yupo tu kwenye Pc, Tv au simu anachat tu! Hii inapunguza sana hisia za mapenzi alizonazo mtu!

Anonymous said...

kuna wengine hata ukiomba wanakunyima....wanaogopa kuchoka, tuwafanyeje?