Sinare Maajar.
Mhe. Benjamin Mkapa akisalimiana na Dr. EllenMkondya-Senkoro, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS mara baada ya kuwasili hotelini tarehe 21 Julai 2012, kuhudhuria
Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI linalofanyika Mjini Washington D.C.
Juu na chini ni Mhe. Benjamin Mkapa akipewa taarifa na Mhe. MwanaidiSinare Maajar, Balozi wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kuwasili Washington D.C kuhudhuria Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI kuanzia Julai 22-28, 2012. Wengine kwenye picha ni Dr. Ellen Mkondya-Senkoro,
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS na picha nyingine ni Ms. Eileen A. Swai, Msaidizi wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa
Juu na chini ni Mhe. Benjamin Mkapa akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Washington Convention Centre Julai 23, 2012 kuhudhuria Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI linalofanyika Mjini Washington D.C.
Juu na chini ni Ma-Champion wa HIV Free-Generation Rais Mstaafu waTanzania Mhe. Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim Chisano wakifuatilia mojawapo ya mikutano ya Kongamano la UKIMWI kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington. Pembeni ni Mhe. Mwanaidi
SinareMaajar, Balozi wa Tanzania Marekani na Dr. Ellen Senkoro wa Taasisi ya Benjamin Mkapa.
Juu na chini ni Ma-Champion wa HIV Free-Generation Rais Mstaafu waTanzania Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim Chisano na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Kenneth Kaunda wakijiandaa kabla ya mjadala kuanza kwenye mojawapo ya mikutano ya Kongamano la UKIMWI kwenye
Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington D.C.
Juu na chini ni Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapaakihitimisha mjadala kuhusu Mpango wa Tohara ya Hiari kwa Wanaume ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwenye mojawapo ya mikutano ya Kongamano la
UKIMWI kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington D.C
Washington
DC;Mhe.
Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaasa
viongozi wa Nchi za Kiafrika kuchukua hatua ya kuhamasisha jamii za kiafrika kuhusu
mpango wa tohara ya hiari kwa wanaume (Voluntary Medical Male Circumcision for
HIV Prevention) kama mojawapo ya njia ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI barani
Afrika.
Mheshimiwa Mkapa aliyasema
hayo alipokuwa anahitimisha mojawapo ya mijadala ya pembeni (Satelite Session) iliyokuwa
inaendelea wakati wa Kongamano la XIX la Kimataifa la
UKIMWI linaloendelea Mjini Washington DC, Marekani ambapo watu takribani 22,000
wanahudhuria. Mjadala huo uliovutia mamia ya wajumbe hususan kutoka Afrika
kuhusu tohara ya hiari kwa wanaume, uliendeshwa na Bi. Brenda Wilson kutoka
Afrika Kusini ulielezea tafiti za
kisayansi kuhusu mpango huo kama njia ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI.
Rais Mkapa alisema mpango
huu ni muhimu kutekelezwa na viongozi wa nchi za Kiafrika kwani imethibitishwa
na tafiti zilizofanyika kwa Waafrika kwamba unapunguza maambukizi kwa asilimia
60, ambapo alisema si jambo dogo katika harakati za kutokomeza UKIMWI. Aliongeza
kuwa ni mpango uliopendekezwa na sisi Waafrika wenyewe na ni wa hiari na hivyo
hakuna atakayeshurutishwa.
“Umebuniwa na nchi za magharibi, lakini
umetafitiwa na kuthibishwa na sisi Waafrika wenyewe, hivyo ni mpango wetu huu”
alisisitiza Rais Mkapa huku akishangiliwa kwa makofi na wajumbe wa mjadala huo.
Ili kutekeleza mpango huu
wa tohara ya hiari kwa mafanikio, Mhe. Mkapa alielekeza mambo matatu. Kwanza nchi
za kiafrika inabidi zitengeneze sera na mikakati madhubuti ya jinsi ya
kukabiliana na janga hili la UKIMWI. Pili mipango na mikakati hiyo imilikiwe na
wananchi wa nchi husika ili wao wenyewe wathibitishe ushiriki wao na sio
kuonekana kama shuruti .Na mwisho mipango na sera za kukabiliana na UKIMWI
itekelezwe kwenye mazingira ya ukweli na uwazi ili jamii za kiafrika ziweze
kutambua athari za janga hili la UKIMWI. Pia serikali nazo zitenge fedha za kusaidia
katika mapambano haya na si kutegemea fedha za wafadhili tu.
“Umefika wakati sasa dunia
nzima ielekeze nguvu zake kwenye kutokomeza ugonjwa huu hatari ambao unaua
maelfu ya watu kila siku” Alisema Mhe. Mkapa na kuongeza kuwa mataifa
mbalimbali duniani hutoa misaada haraka sana mara majanga ya dharura
yanapotokea, kama vile mafuriko, ajali
n.k. Lakini janga la UKIMWI ni kama dharura
inayoendelea na sasa ni wakati muafaka dunia nzima itazame janga la
UKIMWI kama dharura na inayoendelea.
Naye Mwenyekiti mwenza wa
Mpango wa Tohara ya Hiari wa PEPFAR Dkt. Emmanuel Njeuhmeli alithibitisha
tafiti hizo kwa kutoa mfano wa Zimbabwe ambapo maambukizi ya UKIMWI yanakadiriwa
kupungua kwa asilimia 45 ndani ya kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa
mpango huo.
Wengine walioongea katika
mjadala huo ni Angelo Kaggwa (Uganda), Mhe. Dkt. Speciosa Wandira (Uganda), Bi.
Henrica Okondo (Kenya), Chifu Jonathan Mumena (Zambia), Mhe. Oburu Oginga
(Kenya), Mhe. Dkt. Christine Ondoa (Uganda), na Mhe. Blessing Chebundo
(Zimbabwe). Mjadala huo pia ulihudhuriwa na marais wastaafu wanaojishughulisha
na mapambano dhidi ya Ukimwi (
wajulikanao kama Champions for AIDS Free Generation)Mhe. Joachim Chisano, Rais
Mstaafu wa Msumbiji na Mhe. Kenneth Kaunda, Rais Mstaafu wa Zambia
Mhe. Mkapa amehudhuria
Kongamano hili kubwa la UKIMWI kwa mwaliko wa taasisi ya Champions for HIV-Free
Generation inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Mhe. Festus Moghae, ambapo
Mhe. Mkapa ni mmoja wa Ma-Champion nane wa taasisi hiyo.
Kongamano la XIX la
Kimataifa la UKIMWI limeanza Washington DC tarehe 22 Julai hadi 28 Julai 2012
ambapo watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wa Marekani wamehudhuria akiwemo
Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama.
Mwisho
Imetolewa na Ubalozi wa
Tanzania Marekani
Julai 25, 2012
1 comment:
kila ninapo ona kongamano hizi na zinginewe napata kichefu chefu hakuna ukimwi bwana nani kakwambiyeni wameshapata dawa ya ukimwi ila wanataka ngozi nyeusi zipunguwe idadi zo kwa sababu tunazaa sana na duniani tunaonekana tupo wengi na wao wanaona tutawashinda ikiwa tutaelimika,kuchapa kazi kwa bidi etc ndo hiyo hofu yao daima kwamba tuwe chini yao always, so nawashanga sana wakuu wetu lakini kama kuna mnuso wa fungu la pesa waende tu wakachukuwe na kuwazalilisha wananchi wao lakini kubukeni kwamba siku yako ikifika YOU ARE GOING TO BE ANSWERABLE TO YOU LORD KILA ULICHOKIFANYA NA UNACHOKIFANYA HAPA DUNIANI UTAKIJIBU KWA YOUR MAKER LORD/MUNGU WAKO.
usidhani duniani umeletwa bure kutanua kwa ufisadi na udanganyifu..
kizazi hiki kina usomi mwingi lakin na udanganyifu mwingi pia upo kazi kweli kweli
Post a Comment