Hapa ni kwenye ubalozi wa Tanzania Uganda, kama hufahamu chochote kuhusu hii stori ya Chameleone na Big Boss Erick Shigongo, nenda kwenye post zilizopita.
(Picha zote kutoka kwa Bill The African)
Jose Chameleone akiperform wakati wa Usiku wa Matumaini, tamasha lililoweka Historia ya burudani 2012 kwa kuandaliwa na Global Publishers wakishirikiana na wadau wengine.
Kama kumbukumbu zako zipo fresh, muda mfupi baada ya Jose Chameleone kumaliza show yake Uwanja wa taifa July 7 2012 na kufanya kama walivyokubaliana kwenye mkataba, siku mbili baadae stori gazetini ziliandikwa kwamba mwimbaji huyu staa wa Uganda ameshindwa kurudi kwao kutokana na Passport yake ya kusafiria kushikiliwa na Eric Shigongo C.E.O wa Global Publishers walioandaa show hiyo kutokana na kumdai pesa ambazo ilidaiwa alishawahi kulipwa kipindi cha nyuma kuja kufanya show Tanzania lakini hakutokea.
Pamoja na hati yake ya kusafiria kuzuiliwa na Erick Shigongo, aliweza kusafiri kurudi kwao… sasa baada ya kuwa kimya kidogo…… hiki ndicho alichoandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuhusu hiyo ishu.
Kwa ufupi ni kwamba Jose Chameleone amemlalamikia Big Boss Erick Shigongo kuhusu kuendelea kuishikilia Passport yake wakati meneja wake Chemeleone hakuhusika kuchukua hizo dola za Kimarekani 3500 zinazodaiwa kupokelewa na Meneja wa Chameleone kwa ajili ya show iliyopangwa siku nyingi kidogo.
Chameleone amesema aliporudi Uganda alifanikiwa kumkamata na kumpeleka polisi George, mtu ambae ndio anadaiwa kuzichukua hizo pesa akijidai ni meneja wa Chameleone lakini baadae akaachiwa huru ambapo baada ya kuona hivyo ilibidi Chemeleone aende kwa balozi wa Tanzania Uganda ili kupata msaada lakini hakufanikiwa.
Amesema wakati passport yake ilipozuiliwa na Erick Shigongo alikwenda kwenye ubalozi wa Uganda Tanzania na ndio uliomsaidia kumpa Document zilizomuwezesha kurudi nyumbani, kwa sasa amepata mialiko ya shows South Africa, England, Belgium, Norway, Sweeden, Canada n.k lakini hajui itakuaje na anahitaji ushauri kuhusu Erick Shigongo ambae ameshikilia Passport yake kwa zaidi ya mwezi mmoja.
3 comments:
Declare the damn passport lost/stolen/embezzled and get another one.
Law enforcers wanaweza kuchukua passport ya citizen kwa amri ya mahakama. Kisheria ni kosa for a civilian to comfisicate anything from anybody. Hii ni aibu kwa Tanazania for a civilian to be more powerful that criminal justice system. Hata kama huyu musician ana makosa alitakiwa ashitakiwe mahakamani na siyo mdai kuzuia hati yake ya kusafiria.
hapo mkuu shigongo ulichemsha kidipromasia hupaswi kufanya hivyo ni aibu kwa watanzania kwa kumzalilisha star huyo
Post a Comment