HATIMAYE wanachama wa Yanga kwa moyo mmoja usiku wa kuamkia leo
walimchagua mfadhili wao wa zamani, Yusuf Manji kuwa mwenyekiti wa timu
hiyo, lakini majira ya saa nane usiku kabla hajatangazwa zilizuka vurugu
kubwa.
Yanga jana ilifanya uchaguzi wa kujaza nafasi kadhaa ambazo
ziliachwa wazi baada ya mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Llyod
Nchunga, makamu mwenyekiti, Davies Mosha na wajumbe kadhaa kujiuzulu
kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.
Katika uchaguzi huo
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar, zaidi ya
wanachama 2,000 walipiga kura, huku amani ikitawala kuanzia hatua za
awali, lakini hali mbaya ilizuka usiku majira ya saa nane baada ya
walinzi kujisahau na kufungua geti wakifikiri kuwa kura zimemalizika
kuhesabiwa, ndipo mamia ya wanachama waliokuwa nje ya ukumbi huo kuingia
ndani kwa kasi.
Hata hivyo, wasimamizi waliwataka wanachama hao
kutoka nje kwanza kwani kura za mwenyenyekiti zilikuwa bado
hazijahesabiwa, hali iliyozua zogo na kejeli za hapa na pale.
No comments:
Post a Comment