Advertisements

Friday, July 20, 2012

taarifa ya Mkutano


Ndugu wanajumuia na wanachama wa N.E.Umoja Foundation,
Jumuiya inawaajulisheni  kuwa ule Mkutano wa uchaguzi,ulioahirishwa kutokana na sababu zisizoweza kuepukika unatarajiwa kufanyika August 25/26 mwaka huu. Sababu kubwa ya kusogeza mbele tarehe za mkutano huo ni ili kuwapa wanajumuia wenzetu waumini wa dini ya kiislam, kuadhimisha mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani. Nitawajulisheni mahali patakapofanyika mkutano, na muda gani pale matayarisho yatakapokamilika.
Agenda za mkutato ni kama zifuatavyo:
1. Kila Mwanakamati na Mwanachama awe umeshalipa ada ya uanachama ya dola $50.00
Kabla ya mkutano. Yeyote yule atakakuwa hajalipa ada ya uanachama kabla ya siku ya mkutano hatashiriki katika uchaguzi huo kwa maana hatakuwa mwanachama hai wa New England Umoja Foundation, na atakuwa amajiengua kwenye Chama.Form za uanachama zinapatikanawww.newenglandumoja.net, na ada zote za uanachama (check or money order) ziwasilishwe/zitumwe kwa Treasurer, N.E.U Foundation,P.O Box 4262 Springfield MA. 01101.
2. Uchaguzi wa "Board of Directors"
3. Uchambuzi na marekebisho ya N.E Umoja Foundation's bylaws.
4. Kujadili kiundani mikakati na mfumo mzima wa chama chetu na muelekeo wake kwa siku zijazo.
5. Mengineyo..........
Tunawaombea Waislam wote popote walipo duniani mfungo mwema katika mwezi mtukufu, na tuombeane kheri wakati wote huu wakati tunajiandaa na mkutanu huu muhimu.
Asanteni sana.
Salum Salum
Katibu Mkuu
New England Umoja Foundation Inc.

No comments: