Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
MBIO za kuwania urais wa mwaka 2015 zimezidi kuwatesa wanasiasa, baada
ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
kueleza kuwa hajaoteshwa kuwania kiti hicho, huku Mwenyekiti wa CUF
Profesa Ibrahim Lipumba akionya kuwa makundi tofauti yanayowania nafasi
hiyo ndani ya CCM ni hatari.Membe mbali na kusema hajaoteshwa kugombea
urais, ameeleza kuwa ana orodha ya watu kumi na moja wanaomhujumu na
kuonya kuwa ipo siku atawataja kwa majina hadharani.Waziri Membe alitoa kauli hiyo juzi usiku katika Kipindi cha Dakika 45, kinachorushwa na Televisheni ya ITV kila Jumatatu.
Membe alihusisha hujuma hizo na mbio za Uchaguzi Mkuu wa 2015, baada ya kuulizwa ikiwa watu hao wanamfuatafuata kutokana na suala la Uchaguzi Mkuu ujao wa urais.
“Wanajua mambo yote haya, wanaogopa nisiwaguse na wangekuwa na uwezo wangeanza kampeni, labda nioteshwe (urais) na ole wao nikioteshwa ndoto hiyo…” alisema. Waziri Membe na kuongeza:
“Mtu aliye mbaya wako anakuwa na macho matatu. Kwa hiyo kutokana na uwezo wa jicho la tatu anaanza kuzuia lile analoliona lisitokee. Mimi nina macho sita. Nitawataja. Hebu wewe fikiria, kila baada ya miezi miwili naletewa mitego, vituko. Lakini nawaambia Watanzania, waache waseme na mimi ipo siku itakuwa zamu yangu nitawaweka wazi ili kila mtu aelewe.”
“Wasije wakadhani wakijificha kwa wahariri, majumbani kwao ambako ndiyo kuna ofisi zao kwenye ma-godown (maghala) yao ndiyo watakwepa, nitawalipua ili wajue. Ukikaa juu ya nyoka, akigeuka atakuuma tu.”
“Ipo siku nitawaanika hao watu na wapo kumi na moja. Kuna waandishi wa habari mle ndani wawili. Nitawatwanga peupe. Ninyi subirini hata ndani ya Bunge, nitazipangua tuhuma hizo moja baada ya nyingine. Nikimaliza bungeni wajiandae, nitawaanika majina yao, picha zao na mambo yote waliyoandika kwenye magazeti kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wangu kwenye wizara.”
No comments:
Post a Comment