ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 17, 2012

DAKIKA TANO NA ALLY REHMTULLAH - MBUNIFU MAHIRI MITINDO NITE 3 THANKSGIVING SAT, NOV. 24



Ally Remhtullah atakuwa miongoni mwa wabunifu watakaopanda jukwaa Hampton Conference Centre uliopo Washington DC kuonyesha ubunifu wao. Ni katika onyesho la Mitindo Nite msimu wa tatu.

Onyesho hilo lenye theme ‘An African Fashion statement’  litafanyika Novemba 24,2012, ambapo zaidi ya wanamitindo 15 wenye viwango vya kimataifa watapanda jukwaani kuonyesha utajiri halisi wa kiafrika, kupitia wabunifu kazi za wabunifu kadhaa wa kiafrika.

Remhtullah aliingia rasmi kwenye fani ya ubunifu mwaka 2007. Ingawaje tangu mwaka huo amkuwa akifanya kazi zenye viwango vya kimataifa, jambo lilopelekea kualikwa katika nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Afrika.

Baadhi ya nchi alizowahi kuonyesha kazi zake ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda Angola, Malawi, South Africa pamoja na nyingine kibao.

Hadi sasa mbunifu huyu ana jumla ya collection tatu na hivi karibuni anatarajia kuzindua collection yake mpya itakayofahamika kama AR 2013.

Collection zake nyingine zilizotangulia ni pamoja na  Prism break, Temptation na Delictables na Septemba 8, mwaka huu anakuja na onyesho lake la enchanted Jungle kuzindua collection yake ya nne.

Remhtullah anashikilia tuzo kadhaa zinazotambulika katika ubunifu wa mitindo ambapo mwaka jana alitunukiwa tuzo ya mwanamitindo bora wa kiume kwa 2012 katika onyesho la Swahili Fashion week.

Hapa nchini mchango wa Remhtullah unatambulika vilivyo kwani ameshawahi kuwavisha warembo kadhaa katika maonyesho mabalimbali kama vile miss Tanzania na mengine yanayofanana na hilo.

Nilipata wasaa wa dakika tano wa kuongea na mbunifu huyo na haya ndio yalikuwa maongezi yetu

Mwandishi: Uko kwenye maandalizi ya kwenda kuonyesha kazi zako katika jiji la Washington DC. Unaliongeleaje Onyesho hilo?

Remhtullah: Naweza kusema ni miongoni mwa maonyesho muhimu sana kwangu. Kwani watu wa Marekani watapata wasaa wa kuangalia kazi zangu zenye vionjo vya kiafrika. Si hivyo tu nitapata wasaa wa kubadilishana mawazo na wadau wa fashion kutoka katika nchi hiyo yenye wataalamu lukuki.
 
Mwandishi: Fashion inamaanisha nini kwako?

Remhtullah: Fashion ni vazi lolote mtu analoweza kuvaa na kutoka kipekee.Kila mtu anayo style yake binafsi na kila mtu anadefinition yake mwenyewe ya fashion. kwa mimi fashion ni rangi, fashion ni kitu ya kipekee kila mtu anakiona mara mbili.

Mwandishi: Unapangiliaje mavazi yako ya kila siku?

Remhtullah: Kwa kawaida kila sehemu ninayoenda huwa ina vazi lake. Kwa mfano vazi la mskitini ni tofauti na vazi la usiku. vazi la jumatatu ni tofauti na vazi la jumapili.

Mwandishi: Je unakumbuka ni lini ulianza kuzingatia suala la mavazi?

Remhtullah: Nimeanza kufuatilia navyovaa tangu nakumbuka... nilipokuwa mdogo nilikuwa napenda kuenda shopping mwenyewe kwa nguo zangu

Mwandishi: Ni mavazi gani unapendelea hasa unapokuwa kwenye mtoko wa usiku?.

Remhtullah: Nikitaka kutoka ‘out’ usiku huwa napendelea kuvaa  jeans na t-shirt au shati ya mikono mifupi ya slim fit - na raba au viatu za kawaida.

Mwandishi: Kitu gani unakipa kipaombele unapobuni nguo kwenye ‘cloth line’ yako?

Remhtullah: Ninapokuwa nadesign nguo aina yoyote ya label yangu naangalia vitu tofauti tofauti - mtu anayevaa, comfort ya mtu anayevaa na mwisho nataka mitindo yangu iende mbele na sio zakurudia nyuma... ‘fashion is always going ahead’.

Mwandishi: Unaelewa nini kuhusu ‘elegance’na nini siri yake?

Remhtullah: Kwangu mimi elegant ni ‘comfort’, elegant ni ‘simplicity’, elegant ni ‘natural’.

Mwandishi; Ni mbunifu gani unampenda?

Remhtullah: Nawapenda wabunifu wengi sana duniani... nampenda Vivienne Westwood, napenda label za Alexander  Mc queen, napenda nguo za Yves Saint Laurent

Mwandishi; Unachanganyaje mavazi yako?
 
Remhtullah: Binafsi sina formula ya kumix mavazi yangu - Kawaida navaa kitu chochote ninachotamani . Wkati mwingine huwa najali rangi au textures wakati mwingine michoro ya vazi husika.

Mwandishi; Unaweza kuelezea style yako?

Remhtullah: Style yangu huwa inabadilika badilika kila siku .Saa nyingine nakuwa ‘trendy’, saa nyingine nakuwa rock/punk, saa nyingine utaniona niko ‘formal’. Style yangu mara nyingi  inategemea na ‘mood’ yangu tu.

Mwandishi; Umeshawahi kupatwa na ‘wardrobe malfunction’ ?

Remhtullah: Haha...mara nyingi tu - siku moja zip ya suruali yangu ilikatika na kuachia nikiwa kwenye mtoko hiyo moja nyingine  hahahha  nilijimwagia kahawa  kwenye nnguo yangu nikiwa kwenye mkutano mkutano... na siku moja kandambili ilikatika nikiwa naigiza filamu.

Mwandishi; Una dondoo yeyote ya mitindo?

Remhtullah: Usijifekishe kuwa wewe mwenyewe muda wote na kuwa huru. Watu watakujudge kulingana na vazi lako na si vinginevyo.

Mwandishi; Ni nani role model wako katika mavazi?

Remhtullah: Boy George, Brad Pitt, Usher, John Galliano.

Mwandishi; Majarida gani ya mitindo unapendelea kusoma?

Remhtullah: Huwa nasoma sana VIVA, LOOK, inSTYLE, Glamour na mengine mengi.

Mwandishi; Elezea your public style

Remhtullah: Jeans, t-shirt, flip-flops, big shades, chunky rings and a dog-tag on my neck




1 comment:

Anonymous said...

karibu kwa raha zako