ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 22, 2012

JESHI LA POLISI LATAJA ORODHA YA VIJANA 1,446 WALIOTEULIWA KUJIUNGA NA JESHI HILO


JESHI la polisi Tanzania limetoa ajira 1,446 kwa Vijana wa kidato cha nne wa mwaka 2011,kidato cha sita mwaka 2012 na vijana walioko kambi za JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani.

Kati ya hao  951 ni walio hitimu kidato cha nne na sita mwaka 2011/2012 na 495 kwa Vijana waliokuwa katika Kambi za JKT za JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani. 

Maelekezo Muhimu:-
1. Vijana wa kidato cha nne wa mwaka 2011,kidato cha sita mwaka 2012 na vijana walioko JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi baada ya mchakato wa usaili uliokamilika hivi karibuni wanatakiwa kuripoti Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi kati ya tarehe 06/10/2011 na 07/10/2012 kwa ajili ya zoezi la usajili litakaloanza chuoni hapo tarehe 8.10.2012.

2. Vijana hao wanatakiwa kuripoti tarehe 05/10/2012 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kwa ajili ya kuwaandalia usafiri wa kuwapeleka Chuoni.

3. Vijana wanaotoka katika makambi ya JKT yaliyotajwa hapo juu wataripoti kwa makamanda wa Polisi wa mikoa iliyo karibu nao.

Vijana wa kidato cha nne na sita wataripoti kwa makamanda wa Polisi wa Mikoa waliojiandikisha wakati wa zoezi la usaili lililoendeshwa mwezi Julai, 2012.

4. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Chuo cha Polisi Moshi

5. Vijana hawa wanatakiwa kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
a) Vyeti vyao vyote vya masomo(Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

b) Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
c) Chandarua
d) Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
e) Pasi ya Mkaa
f) Ndoo moja.1
g) Pesa kidogo ya kujikimu.
6. Kwa mujibu wa kanuni za chuo ni marufuku kufika chuoni na simu ya mkononi, atakayepatikana na simu atafukuzwa chuoni hapo. Chuo kitaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano. 
7. Hakikisha jina lako liko kwenye orodha hii. Jeshi la Polisi
halitahusika na gharama zozote kwa atakaye kiuka maagizo haya.
KUPATA ORODHA KAMILI NA MASHARTI BOFYA HAPA....POLISI

No comments: