Kuhojiwa kwa Lissu kunaongeza majina mazito ya waliokwisha kuhojiwa wakiwamo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi
.
Mchakato wa kuwahoji ulianza tangu wiki iliyopita huku wengine wakiwa tayari wamepokea wito kwenda katika mahojiano na kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo (CCM), Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan ngwilizi.
Taarifa zinasema kuwa Lissu alianza kuhojiwa kwa saa tatu na Kamati ya Haki, Maadili na Mamlaka ya Bunge kuhusiana na kauli yake kuwa uteuzi wa majaji wa hivi karibuni haukupitia katika taratibu za kiuteuzi, ikiwemo Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Mahojiano hayo yalifanyika katika jengo la utawala na kisha kufuatiwa na mahojiano kwenye Kamati ndogo ya Ngwilizi.
Habari zinasema kuwa katika kikao kilichofanyika katika moja ya vyumba vya ukumbi wa Pius Msekwa, Lissu alihojiwa kwa saa 2.30, jambo lililofanya Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM) ambaye alipangiwa kuhojiwa siku hiyo kushindwa kuhojiwa.
Hali hiyo ilimfanya Keissy kupangiwa siku ya jana. Jana Keissy alionekana karibu na jengo la Pius Msekwa, akisubiria kuitwa kuhojiwa.
Wengine waliokuwa wakisubiri kuhojiwa jana ni Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe (CCM) na Mbunge wa Viti Maalum, Sara Msafiri (CCM).
Taarifa pia zinasema kuwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, naye amekwisha kuhojiwa na kamati hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, baadhi ya wabunge akiwemo Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-Chadema), John Mnyika (Ubungo-Chadema) na Sulemain Zedi (Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini) wamepewa barua za wito wa kwenda katika kamati hiyo.
Wengine waliopata wito wa kuitwa kuhojiwa ni Yusuph Nassir (Korogwe Mjini-CCM), Charles Mwijage (Muleba Kaskazini-CCM), Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Diana Chilolo.
Sakata hilo lilianza baada ya baadhi ya wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2012/13 kudai kuwa kuna wenzao wamehongwa na makampuni ya mafuta ili kushinikiza Waziri Muhongo na Maswi wong'olewe katika nafasi zao.
Shinikizo hilo linadaiwa kuwa lilitokana na wizara hiyo kuipa zabuni kampuni ya Puma Energy kwa ajili ya kuiuzia serikali mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya IPTL.
Baada ya kutolewa madai hayo, Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (CCM), alitoa hoja akitaka kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kutokana na wajumbe wake kutuhumiwa kuhongwa.
Hadidu za rejea za kamati hiyo ni kuchunguza tuhuma kama baadhi ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini walijihusisha na vitendo vya rushwa au la.
Alisema kamati hiyo imeundwa kwa mujibu wa Kanuni ya 114 (18) kwa lengo la kuwezesha uchunguzi kufanyika haraka.
“Ili suala hili liweze kushughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi kamati ndogo inatakiwa kufanya mambo yafuatayo; kwanza ni kukutana na kukubaliana namna bora ya kushughulikia suala hili pamoja na mapendekezo yaliyotolewa,” alisema Makinda.
Pia alisema mambo mengine ambayo kamati hiyo inatakiwa kuyafanya ni kupitia kumbukumbu rasmi za Bunge za Julai 27 na 28, mwaka huu ambapo bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliwasilishwa ili kupata picha ya namna mjadala mzima ulivyoendeshwa.
Spika Makinda aliongeza kuwa, mambo mengine wanayotakiwa kuyafanya ni kuwaita na kuwahoji mashahidi ambao wataisaidia kamati kujua ukweli wa tuhuma hizo.
Alimtaja Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ambaye katika mkutano wake na waandishi wa habari alitaja majina ya wabunge kadhaa wenye mgongano wa kimaslahi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mashahidi wanaopaswa kuhojiwa.
Alisema wengine wanaoweza kuwaita ni Waziri wa Nishati na Madini ambaye alibainisha kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hotuba yake.
“Wabunge wote waliochangia hotuba ya Nishati na Madini na kutoa tuhuma dhidi ya wabunge wengine kujihusisha na vitendo vya rushwa katika wizara hiyo na mbunge mwingine yeyote anayeweza kuisaidia kamati katika uchambuzi wa suala hili na kisha kuwasilisha taarifa kwa Spika juu ya ushauri na mapendekezo ya hatua zaidi,” alisema.
Alisema anamini kuwa wabunge wote ambao walisema kuwa wana ushahidi ama walimtaka Spika ataje majina sasa watakwenda katika kamati hiyo kutaja majina hayo.
Pia aliwataka wabunge watakaoitwa kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo na kwamba wanaweza kutumia watu wengine wanaofahamu kuwasaidia.
Kamati hiyo ilipewa wiki mbili kukamilisha kazi hiyo na baada ya kukamilisha itawasilisha taarifa yake kwa Spika.
Wajumbe wa kamati hiyo na majimbo yao katika mabano ni Kapteni John Chiligati (Manyoni Mashariki-CCM); Riziki Omar Juma (Viti Maalum-CUF); Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema) na Gosbert Blandes (Karagwe-CCM).
Kamati ndogo ya Bunge iliyoundwa na Spika, Anne Makinda, kuchunguza tuhuma za baadhi ya wabunge kuhongwa na kampuni za mafuta, imeendelea kuwahoji baadhi ya wabunge, safari hii Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye Spika alimtaja kama shahidi namba moja alihojiwa Jumamosi iliyopita.
Kuhojiwa kwa Lissu kunaongeza majina mazito ya waliokwisha kuhojiwa wakiwamo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi.
Mchakato wa kuwahoji ulianza tangu wiki iliyopita huku wengine wakiwa tayari wamepokea wito kwenda katika mahojiano na kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo (CCM), Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan ngwilizi.
Taarifa zinasema kuwa Lissu alianza kuhojiwa kwa saa tatu na Kamati ya Haki, Maadili na Mamlaka ya Bunge kuhusiana na kauli yake kuwa uteuzi wa majaji wa hivi karibuni haukupitia katika taratibu za kiuteuzi, ikiwemo Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Mahojiano hayo yalifanyika katika jengo la utawala na kisha kufuatiwa na mahojiano kwenye Kamati ndogo ya Ngwilizi.
Habari zinasema kuwa katika kikao kilichofanyika katika moja ya vyumba vya ukumbi wa Pius Msekwa, Lissu alihojiwa kwa saa 2.30, jambo lililofanya Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM) ambaye alipangiwa kuhojiwa siku hiyo kushindwa kuhojiwa.
Hali hiyo ilimfanya Keissy kupangiwa siku ya jana. Jana Keissy alionekana karibu na jengo la Pius Msekwa, akisubiria kuitwa kuhojiwa.
Wengine waliokuwa wakisubiri kuhojiwa jana ni Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe (CCM) na Mbunge wa Viti Maalum, Sara Msafiri (CCM).
Taarifa pia zinasema kuwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, naye amekwisha kuhojiwa na kamati hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, baadhi ya wabunge akiwemo Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-Chadema), John Mnyika (Ubungo-Chadema) na Sulemain Zedi (Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini) wamepewa barua za wito wa kwenda katika kamati hiyo.
Wengine waliopata wito wa kuitwa kuhojiwa ni Yusuph Nassir (Korogwe Mjini-CCM), Charles Mwijage (Muleba Kaskazini-CCM), Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Diana Chilolo.
Sakata hilo lilianza baada ya baadhi ya wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2012/13 kudai kuwa kuna wenzao wamehongwa na makampuni ya mafuta ili kushinikiza Waziri Muhongo na Maswi wong'olewe katika nafasi zao.
Shinikizo hilo linadaiwa kuwa lilitokana na wizara hiyo kuipa zabuni kampuni ya Puma Energy kwa ajili ya kuiuzia serikali mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya IPTL.
Baada ya kutolewa madai hayo, Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (CCM), alitoa hoja akitaka kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kutokana na wajumbe wake kutuhumiwa kuhongwa.
Hadidu za rejea za kamati hiyo ni kuchunguza tuhuma kama baadhi ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini walijihusisha na vitendo vya rushwa au la.
Alisema kamati hiyo imeundwa kwa mujibu wa Kanuni ya 114 (18) kwa lengo la kuwezesha uchunguzi kufanyika haraka.
“Ili suala hili liweze kushughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi kamati ndogo inatakiwa kufanya mambo yafuatayo; kwanza ni kukutana na kukubaliana namna bora ya kushughulikia suala hili pamoja na mapendekezo yaliyotolewa,” alisema Makinda.
Pia alisema mambo mengine ambayo kamati hiyo inatakiwa kuyafanya ni kupitia kumbukumbu rasmi za Bunge za Julai 27 na 28, mwaka huu ambapo bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliwasilishwa ili kupata picha ya namna mjadala mzima ulivyoendeshwa.
Spika Makinda aliongeza kuwa, mambo mengine wanayotakiwa kuyafanya ni kuwaita na kuwahoji mashahidi ambao wataisaidia kamati kujua ukweli wa tuhuma hizo.
Alimtaja Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ambaye katika mkutano wake na waandishi wa habari alitaja majina ya wabunge kadhaa wenye mgongano wa kimaslahi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mashahidi wanaopaswa kuhojiwa.
Alisema wengine wanaoweza kuwaita ni Waziri wa Nishati na Madini ambaye alibainisha kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hotuba yake.
“Wabunge wote waliochangia hotuba ya Nishati na Madini na kutoa tuhuma dhidi ya wabunge wengine kujihusisha na vitendo vya rushwa katika wizara hiyo na mbunge mwingine yeyote anayeweza kuisaidia kamati katika uchambuzi wa suala hili na kisha kuwasilisha taarifa kwa Spika juu ya ushauri na mapendekezo ya hatua zaidi,” alisema.
Alisema anamini kuwa wabunge wote ambao walisema kuwa wana ushahidi ama walimtaka Spika ataje majina sasa watakwenda katika kamati hiyo kutaja majina hayo.
Pia aliwataka wabunge watakaoitwa kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo na kwamba wanaweza kutumia watu wengine wanaofahamu kuwasaidia.
Kamati hiyo ilipewa wiki mbili kukamilisha kazi hiyo na baada ya kukamilisha itawasilisha taarifa yake kwa Spika.
Wajumbe wa kamati hiyo na majimbo yao katika mabano ni Kapteni John Chiligati (Manyoni Mashariki-CCM); Riziki Omar Juma (Viti Maalum-CUF); Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema) na Gosbert Blandes (Karagwe-CCM).
No comments:
Post a Comment