ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 22, 2012

Mdau Ally Kindoile apenya usaili KRFA


 Ally Kindoile
 Kindoile akihojiwa baada ya usajil
 Kindoile alkiwa na wagombea wengine
 Mmoja wa wagombea akiwa na nyaraka zake kabla ya usaili
waandishi wa habari
Uchaguzi  sasa kufanyika Septemba 9
USAILI  kuwania nafasi ya uongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA), umefanyika mapema leo Agosti 22,  chini ya Mwenyekiti wake Dr. Haule na kushuhudia viongozi mbalimbali wakichaguliwa huku mdau wa michezo na aliekuwa Mjumbe wa Villa Squad, Ally Kindoile, kupenya kwenye usaili huo.
 
Katika usaili huo ulioshuhudiwa na wadau mbalimbali wa michezo, ulifanyika katika ofisi za Manispaa ya Moshi,  ambapo nafasi ya Mwenyekiti waliopita ni pamoja na Godluck Moshi  na Charles Mchau, Makamu Mwenyekiti Shaban Mwalimu  na nafasi ya Katibu Mkuu msaidizi kwenda kwa Ally Kindoile.
 
Aidha nafasi zingine walizopita wadau hao wa soka wa Mkoa wa Kilimanjaro, majina na nafasi zao kwenye mabano ni Kusianga Kiata (Mhani), Distin Kilua  na Abdala Husein (Wajumbe Mkutano Mkuu).
 
Wengine ni Keneth Essau  na Amri Kiula (Wawakilishi wa Vilabu), Denis Joseph Msemo, Cuthbert Mushi  na Nassor Muchi (Wajumbe Kamati  ya  utendaji) na Salma Omari Mndaira (Mwakilishi TWFA).
 
Katika hatua hiyo, Uchaguzi wake unatarajia kufanyika Septemba 9,Ulili, Mkoani humo.
 
Hata hivyo, Ali Kindoile alipozungumza na waandishi wa Habari, muda mfupi baada ya usaili huo, alishukuru kwa kupita kwake na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuinua soka la Mkoa  huo, ambapo mipango yake mbalimbali anatarajia kushirikiana na wagombea wenzake pindi watakapofanikiwa kwa pamoja kupata nafasi hiyo hiyo Septemba 9.
 
“Tunaomba ushirikiano na umoja ili kufika mbali katika soka letu, umoja wetu ndio tutasaidia soka la mkoa huu” alisema Kindoile.
 
Kindoile licha ya kuwa mdau wa michezo, aliwahi kuchezea timu mbalimbali zikiwemo Simba B na Idrisa Fc, kwa sasa ni mdau mkubwa wa timu ya Kilimanjaro Rangers ya mkoani humo na amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia vijana kwenye soka.
 
Uchaguzi huo awali ulitakiwa kufanyika Agosti 28,  ambapo sasa umesogezwa mbele mpaka hapo Septemba 9.

No comments: