Sunday, August 19, 2012

Mganga anaswa na mabomu


Mganga wa kienyeji  Msindi Masaki  mkazi wa kijiji cha Ilolangulu mkoani Tabora, ametiwa mbaroni na polisi baada ya kunaswa na mabomu  manne aliyokuwa ameyafukia ardhini nyumbani kwake.

Kituo cha ITV kilimnukuu Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Anthony  Rutashuburugukwa, akisema  alikamatwa na mabomu hayo ya kijeshi kinyume cha sheria  akiwa kwenye harakati za kuyatumia kufanya uharifu na utekaji  watu katika moja ya minada inayoendeshwa vjijini mkoani humo.

Kamanda  alisema  inawezekana kuwa mabomu haya yameagizwa kutoka nchi jirani kwa lengo lakufanyia uhalifu  na kwamba mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote

Rutashugurubukwa alisema  pamoja na mganga huyo watuhumiwa  wengine 22 walikamatwa kwenye msako wa  wahalifu uliofanyika mjini hapo na vitu mbalimbali vimekamatwa zikiwemo samani mbali mbali ,  televisheni, redio, nondo, vitanda,  gongo na  pikipiki moja ambayo inachunguzwa uhalali wake kutokana na dereva wake  kukimbia baada ya kusimamishwa na polisi usiku.

Aliwataka wananchi walioibiwa mali zao  kufika kituoni hapo kufanya utambuzi.

Aidha Kamanda  Rutashuburugukwa alisema  katika kukamatwa wahalifu imepatikana silaha moja aina ya gobole linalotumia risasi za bunduki ya shotgun na maganda sita na risasi tatu zikiwa hazijatumika.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments: