ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 22, 2012

MSAADA KWENYE TOPE

Mimi naitwa Matunda Malaika ni Mtanzania naeishi Washington State, nipo hapa Marekani tangia 1995 nilianzia maisha Wichita na ndipo mwaka 2010 nilipohamia hapa Seattle, WA.

Tangia nimekuja hapa Marekani kuna maneno mawili ambayo kusema ukweli yananitatiza sana neno MNUGU na MPOPO najua sisi Watanzania mmarekani mweusi tunamuita Mnugu na Mwafrika wa Afrika Magharibi tunamuita mpopo, kinachotitatiza ni maana halisi ya maneno hayo na asili yake.

naomba msaada mninasue kwenye tope unaposema MNUGU asili ya neno ni wapi na kwanini Mmarekani mweusi tuna muita MNUGU? na naomba asili ya neno MPOPO kwanini watu wa Afrika Magharibi tunawaita WAPOPO? Asante.

Mdau Matunda Malaika,
Washington, State.

4 comments:

Anonymous said...

Ni vema na wewe ukatueleza kwanza kwanini unaitwa Matunda Malaika na asili ya majina haya ni wapi hapa Tanzania.

Anonymous said...

gojea nikufafanulie kwanini mmarekani mweusitunamwita mnugu,ilinikifupi kumtamka mtubila kugielewa kwamfano wewe hukopamoja nammarekani ,badala ya kumwabia huyummarekani unawezakusema mnugu.====WAPOPO NI VILEVIE

Anonymous said...

Kuhuliza sio ujinga,ngoja nikufahamishe asili ya maeno haya, "Mnugu" jina hili lilianzishwa na mMarekani mmoja aliyekuja kutoa hotuba mbele ya jumuiya ya wa Tanzania kule Washington, wakati w hotuba yake alianza na kusema "Thank you Wanungu zangu,ikiwa na maana ya asanteni sana wandugu zangu , ndipo watu walicheka sana, na kulichukua hilo neno,
"Mpopo" hili jina limetokea kwa mabeach boy wa kiTanzania, kwa nchi nyingine jina hili linamuhusisha sana MNigeria na mNghana, ilikua kila nchi anayoyo dondoka mTanzania, lazima mtu mweusi atakayekutana naye ni mnigeria au Mghana,ndipo wakwa wnese hawa watu ni kama Popo kila sehemu wapo,ndipo lilipoanza kutumika wakati wakiwa pamoja nao ili wasijue kama walikua wanawaongelea wao,,, kuna majina mengine kama wabangubangu,(mozambique0 wakunjani, {wazulu} wazimzim,(Wazimbabwe)na wengine wengi tu.

Anonymous said...

mimi ndio nilioanzisha jina la mnugu miaka ya tisini,kabla sijikueleza nililipata wapi naomba tuambie mkasa uliokupata hadi unataka kuyajua haya