Wafanyikazi wa migodi nchini Afrika Kusini wameanza kurudi mmoja mmoja katika migodi ya dhahabu nyeupe, platinum, ambako polisi waliwafyatulia risasi wenzao na kusababisha vifo vya watu 34 Alhamisi iliyopita.
Hata hivyo idadi ya wachimba migodi hao haijatosha kiasi cha shughuli za uchimbaji migodi kuendelea kikamilifu.Kampuni pia ilitangaza kwamba imetenga muda wa wafanyakazi wote kurudi kazini, na kuongezea muda huo hadi Jumanne.
Imetisha kwamba watakaoshindwa kufanya hivyo, basi watafutwa kazi.
Rais Jacob Zuma alitangaza wiki nzima ya maombolezi kufuatia vifo vya wachimba migodi waliouawa.
Vile vile alitaka uchunguzi kamili kufanyika.
No comments:
Post a Comment