Timu za Simba na Mtibwa zilitinga katika fainali ya Ligi ya Super8 baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Simba iliyochezesha kikosi cha vijana watupu, iliifunga Azam iliyojaza wakali kibao wa kikosi cha kwanza kwa mabao 2-1 jioni katika mechi iliyotanguliwa na ushindi mzito wa Mtibwa wa 5-1 dhidi ya Jamhuri ya Pemba.
Matokeo hayo yanamaanisha kwamba Simba na Mtibwa zitakutaka katika fainali keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuwania zawadi ya kwanza ya michuano hiyo maalum ya kujiandaa na msimu mpya, ambayo ni Sh. milioni 40 kutoka BancABC, waandaaji michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Mshindi wa pili wa michuano hiyo, atapata zawadi ya Sh. milioni 20. Timu mbili zilizoiishia hatua ya nusu fainali, Azam na Jamhuri, kila moja itapata Sh. milioni 15 wakati zilizobaki za Super Falcon, Zimamoto na Mtende za Zanzibar pamoja na Polisi Morogoro ya Bara, zote kila moja itapata Sh. milioni 5.
Simba ilipata goli lake ya kwanza mapema katika dakika ya 2 kupitia kwa Rashid Ismail kufuatia pasi safi ya Miraji Adam, ambalo lilidumu hadi wakati wa mapumziko na wakaongeza la pili katika dakika ya 55 kupitia kwa Edward Christopher aliyefunga nja ya penalti iliyotolewa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es salaam baada ya mfungaji huyo kuangushwa na beki wa Azam, Luckson Kakolaki, ndani ya boksi. Lilikuwa ni goli la tano katika mechi nne za michuano huyo kwa Edward.
Azam iliyokuwa na wachezaji wa timu A kama Kipre Tcheche, Gaudence Mwaikimba, Said Morad, Jabir Aziz, Abdulhalim Humoud na Abdi Kassim walipata goli la kufutia machozi katika dakika ya 71 kupitia kwa Zahor Pazi aliyefunga kwa kutumia makosa ya mabeki wa Simba kujichanganya.
Kikosi cha Simba kilikuwa: Abuu Hashim, Miraji Adam, Omar Salum/ William Lucian (dk.80), Hassan Isihaka, Hassan Khatib, Said Ndemla, Haruna Athuman, Dullah Seseme, Edward Christopher/ Rama Mzee (dk. 84) na Frank Sekule/ Ibrahim Khatib (dk. 64).
Azam: Jackson Wandwi, Ibrahim Chimwanga, Samir Nuhu, Said Morad, Abdulhalim Humoud, Sunday Frank/ Kevin Friday (dk. 59), Jabir Aziz/ Himid Mao (dk. 34), Abdi Kassim 'Babi', Kipre Tchetche/ Khamis Mcha (dk. 61) na Gaudence Mwaikimba/ Zahor Pazi (dk. 66).

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment