Mbuyu Twite akisaini Yanga
Uongozi wa Klabu ya Simba jana uliwasilisha barua ya pingamizi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikipinga usajili wa mabeki wawili, Kelvin Yondani na Mbuyu Twite, waliosajiliwa na mahasimu wao Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Bara.
Simba pia imeweka pingamizi ikitaka wajumbe wanaounda Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji iliyoko chini ya mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa, ikitaka wasihudhurie kikao cha kusikiliza pingamizi hilo kwa madai kwamba wajumbe wake wana 'mapenzi' na mahasimu wao Yanga.
Jina la Yondani limo katika usajili wa Simba na Yanga wakati Twite jina lake liko kwenye orodha ya wachezaji wa Yanga tu.
Akizungumza jana, Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa klabu yake imefikia maamuzi ya kuweka pingamizi dhidi ya Yondani kwa sababu inaamini mchezaji huyo ni mali yake kwani wana mkataba naye ambao aliusaini Desemba mwaka jana na makosa ya kisarufi yasiufanye mkataba huo kutotambuliwa.

Kelvin Yondani akisaini Yanga
Kamwaga alisema pia Simba imemuwekea Twite pingamizi kwa sababu ya 'rafu' waliyofanyiwa na Yanga katika kumsajili mchezaji huyo ambaye awali walishamsajili.
Alisema kwamba mabingwa hao wa Ligi ya Bara pia wameitaka TFF iteue wajumbe wengine huru ambao si wanachama au waliowahi kuwa viongozi wa Yanga kujadili pingamizi lao kwa sababu hawana imani na wajumbe waliopo hivi sasa.
Mbali na Mgongolwa ambaye ni mwanachama wa Yanga, wajumbe wengine ambao wako kwenye kamati hiyo na Simba haina imani nao ni waliokuwa wenyekiti wa Yanga kwa nyakati tofauti, Imani Madega na Lloyd Nchunga.
Wengine wanaounda kamati hiyo ni Makamu Mwenyekiti, Hussein Mwamba ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, Omar Gumbo (Makamu Mwenyekiti wa Simba wa zamani) na Venance Mwamoto.
Licha ya Simba kumsainisha Twite, lakini jina lake hawakulituma katika orodha ya wachezaji iliyowasajili.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah aliithibitishia NIPASHE kupokewa kwa pingamizi hilo.
TFF ilitoa siku saba kuanzia Agosti 15-22 kwa ajili ya kupokea mapingamizi ya usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu mpya wa 2012/13.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake