Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) limesema kuwa litamkatia tiketi maalumu mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ili arejee jijini Dar es Salaam Jumatatu akitokea Botswana ambako timu ya taifa ya Uganda (Cranes) imekwenda kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa.
Okwi alikuwa mmoja wa nyota wa Cranes walioondoka jana asubuhi kuelekea Gaborone kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki ambao Uganda waliomba katika maandalizi ya mechi za kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, aliiambia NIPASHE kuwa FUFA wamewatumia barua ya pili ya kumuomba Okwi kuichezea timu hiyo huku ikithibitisha kwamba nyota huyo atarejea Dar es Salaam Jumatatu kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Bara.
Mtawala alisema kwamba FUFA pia iliwaomba radhi Simba kwa kutaka kumtumia Okwi kwenye mchezo huo lakini akaongeza kuwa taarifa za kusogezwa mbele kwa ligi kuu ya Tanzania Bara kuliwafanya Uganda wamtumie mshambuliaji huyo.
"Walisema kwamba mechi hiyo ni muhimu na Okwi ataendelea kujifua na wameahidi watamsafirisha peke yake wakati wachezaji wengine watabakia huko wakisubiri kuondoka pamoja," alisema Mtawala.
Okwi, Hamis Kiiza wa Yanga na Joseph Owino wa Azam waliitwa na kocha wa Cranes, Bobby Williamson kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Malawi iliyokuwa kwenye kalenda ya FIFA Jumatano ya Agosti 15 mwaka huu lakini haikufanyika kwa kilichoelezwa Malawi kuhofia ugonjwa wa Ebola uliopiga Uganda.
Hata hivyo, Kiiza alirejea nchini na kuungana na wenzake kwa ajili ya safari yao ya Kigali, Rwanda.
Okwi hajafanya mazoezi na Simba tangu msimu wa ligi uliopita ulipomalizika ambapo pia hakuweza kuichezea timu yake hiyo kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) baada ya kuondoka kwa nia ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Austria.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake