Friday, August 24, 2012

'Wavamizi' 100 wa ardhi wakamatwa K'ndoni, nyumba 500 zavunjwa



Baadhi ya wakazi wa eneo la wazi lililovamiwa na kumilikiwa isivyo halali na watu maeneo ya Madale, Kinondoni Dar es Salaam, ambako Polisi walikuwa wakiendesha oparesheni ya kuvunja nyumba na vibanda vyao, wakiwa wamewekwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini.
Askari Polisi akiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya kinondoni wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi akiangalia badhi ya vifaa vilivyokuwemo ndani ya moja ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi, akimuongoza mmoja wa vijana waliokuwa wakiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni juzi.
Kwa picha zaidi na habari bofya read more
Mmoja wa askari Polisi, akimuongoza kijana mwingine aliyekuwa akiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni juzi.
Askari Polisi wakiwa wamesimama sehemu kilipobomolewa moja ya vibanda juzi, vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi ya wananchi maeneo ya Madale, Kinondoni, Dar es Salaam.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo lililovamiwa maeneo ya Madale Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Dereva wa gari la Jambo Leo, Privatus Kachema, akiangalia zoezi la uvunjaji wa nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam juzi.
Moja ya nyumba zilizovunjwa katika oparesheni ya uvunjaji wa nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi la Madale juzi.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo hilo la wazi.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likiendelea kuvunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo.
Askari Polisi na Mgambo wa Manispaa ya Kinondoni, wakikagua moja ya kibanda kabla ya kuvunjwa na tingatinga la Manispaa hiyo, wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi na mgambo wa Manispaa ya Kinondoni wakiangalia tingatinga la Manispaa hiyo, wakati likivunja nyumba na vibanda vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi ya wananchi wengine maeneo ya Madale wilayani humo.


Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.

Moja ya bango lililokutwa limeandikwa na watu hao, likiwa na ujumbe uliokuwa ukimshutumu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela na OCD wake.
Mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa wavamizi wa eneo hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Said, akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kupata athari kichwani wakati alipokuwa akiwekwa chini ya ulinzi na askari Polisi kwenye maeneo hayo. Picha zote na Kassim Mbarouk wa Bayana Blog


Zaidi  ya wananchi 100 wamekamatwa katika Operesheni iliyoanza juzi ya kuwaondoa watu waliovamia maeneo yasiyo yao, inayoendeshwa katika eneo la Nakasangwe, Kata ya Wazo, wilayani Kinondoni chini ya Kamanda Charles Kenyela ambaye pia ni Kamanda wa kipolisi wa mkoa huo, kwa makosa ya kuvamia maeneo ya watu, kulishambulia jeshi la polisi wakati likiingia kutekeleza zoezi hilo kwa kutumia silaha za jadi ambazo ni panga, shoka, upinde na mawe pamoja na kukutwa na pombe haramu ya gongo.

Aidha, zaidi ya makazi ya kudumu na siyo ya kudumu 500 yamebomolewa kufikia jana katika operesheni hiyo.

Kamanda Kenyela aliiambia NIPASHE jana kwamba operesheni hiyo haikupata upinzani wowote kwa siku ya jana.



“Leo (jana) tumeingia hapa Nakasangwe tukianzia kwenye kitongoji cha Kaza Roho kwa amani, na hatukupata mtu wa kutuzuia, kuturushia chochote na kwa kweli kuko shwari kama unavyoona.Wengi wa wananchi waliopo wanatoa vifaa vyao na sisi hatuna tatizo la kumzuia mtu anayetoa mali yake, kwa kuwa lengo letu sisi kama tulivyokuwa tumewaambia toka awali, ni kuwa hatutaki watu wa kuvamia maeneo ya wenzao,” alisema.

Alisema polisi jana haikurusha bomu hata moja la kutoa machozi wala risasi katika eneo hilo kwa kuwa hali ilikuwa shwari.

Kamanda Kenyela alisema wakati wa operesheni hiyo jana walifanikiwa kuvunja nyumba moja ambayo iligundulika kuwa ndiyo ilikuwa inatumiwa na wavamizi kama Ofisi ya Serikali ya Mtaa huo katika kitongoji cha Kaza Roho ambapo walikuta mihuri, nakala ya hati za mauziano ya maeneo ya watu zilizokuwa zikisimamiwa na serikali hiyo bandia, nakala ya barua ‘feki’ zilizokuwa zikiwatambulisha wananchi wa maeneo hayo kama wakazi halali pamoja na ubao wa matangazo.

Aidha alisema kwamba waliweza kuvunja vile vile shina la wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) la Kinondo C lililokuwa limejengwa kwenye eneo la mmiliki aliyekuwa amevunjiwa nyumba yake na wavamizi, kufukuzwa  na mbuzi wake 50 walichinjwa na wavamizi hao.

Alisema polisi pia wamewakamata wanawake watatu na dalali wao waliokuwa wameletwa kuonyeshwa eneo la kununua ambalo linamilikiwa na mtu mwingine.

Kamanda Kenyela aliwaasa wananchi wanaomiliki maeneo yao katika eneo hilo na maeneo mengine jijini Dar es salaam, kutoyaacha kwa muda mrefu bila kuyatembelea wala kuyaendeleza kwani yanapobaki hivyo, yanageuka kishawishi kwa baadhi ya watu kudhani hayana wenyewe na hivyo kuyavamia.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake