ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, August 21, 2012
ULIMBOKA AIBUKA KANISANI UBUNGO NA KUSEMA HAYA
*Atoa sadaka maalumu, awashukuru Watanzania *Adai unyama aliofanyiwa anamuachia Mungu
HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt.Steven Ulimboka, ameibuka na kusema kitendo cha kinyama alichofanyiwa na watu waliomteka anamuachia Mungu.
Dkt.Ulimboka aliyasema hayo Dar es Salaam juzi alipokwenda kutoa sadaka ya shukrani na familia yake kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo.
Katika ibada hiyo, Dkt.Ulimboka ambaye pia alisindikizwa na ndugu zake wa karibu, alimshukuru Mungu kwa kumpigania maisha yake na kurudi salama, madaktari wenzake na Watanzania wote kwa maombi yao ambayo yamemwezesha apone haraka.
Kabla ya kutoa sadaka maalumu, Dkt. Ulimboka aliomba kusomewa kitabu cha Zaburi 124 isemayo; “Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israel na aseme sasa, kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, wanadamu walipotushambulia, wangalitumeza hai”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment