ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 20, 2012

AJALI ZA BARABARANI HUSABABISHWA NA MAKUSUDI NA MICHEZO KAMA HII HAPA.

AJALI nyingi za barabarani nchini husababishwa na madereva wazembe wasio zingatia sheria za matumizi sahihi ya barabara. Miongoni mwa ajali hizo nyingi husababishwa na madereva hao kuovatake magari mengine katika kona au milima kama basi hili linavyofanya katika kona ya Lugalo mkoani Iringa. Madereva “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
Basi hili linguine nalo lilikuwa linafanya makopsa hayo hayo ya kulipita gari linguine katika miinuka na kona kali za mlima Kitonga.
Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Iringa, akiwepo RTO, SP. Pamphil Honono (kushoto) walimuona na kumsimamisha dereva wa basi hilo. Matukio haya yanatokea ndani ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa. 
Dereva huyo alikuwa ni Issack Gerald Nyamaiswe Mkazi wa Mjini Dodoma.
Nahapa Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani akimwandikia Notfication dereva huyo. Picha kwa hisani ya This Day

No comments: