ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 24, 2012

JOHN TERRY AASTAFU SOKA LA KIMATAIFA


JOHN TERRY amestaafu kutoka kuichezea England kuanzia leo.Nahodha huyo wa zamani wa England anaamini FA wameiweka nafasi yake katika njia panda.Alisema: “Leo natangaza kustaafu kwangu kutoka kwenye soka la kimataifa. Ningependa kuwashukuru makocha wote walionichagua na kunichezesha kwa mara 78. Nimekuwa na wakati mzuri katika kucheza kwa pamoja na wachezaji wote niliowahi kuwa nao pamoja kwenye timu ya taifa, ningependa kuwashukuru wao, mashabiki na familia yangu kwa sapoti na kunijaza nguvu wakati niikitumikia timu yangu ya taifa."Kuiwakilisha na kuiongoza nchi yangu ndio kitu nilichokuwa nakiota tangu mdogo na kiukweli imekuwa heshima kubwa kwangu."Mara zote nimekuwa nikijitoa kwa yote na inaniumiza sana moyo wangu kufanya uamuzi huu."Napenda kumtakia kheri Roy Hodgson na timu kupata mafanikio."Nafanya uamuzi huu leo kabla ya usikilizwaji wa kesi yangu iliyo mbele ya FA kwa sababu nadhani, katika kuendeleza mashtaka dhidi yangu ambayo nilishaonekana sina makosa mahakamani, kumeiweka nafasi yangu katika timu ya taifa kuwa njia panda. “Sasa naangalia mbele kuichezea timu ya Chelsea FC na kupigania makombe ya nyumbani na ulaya na ningependa kuwashukuru mashabiki wa klabu yangu kwa sapoti yao endelevu.

No comments: