Rais wa TBF,Phares Magessa
Awali tulitoa taarifa ya ujio wa makocha wa kikapu toka Marekani, Kocha Albert Sokaitis (Kocha Mkuu) na Kocha Mkuu Msaidizi Jocquis L. Sconiers ambao ilikuwa wafike nchini leo tarehe 21/09/2012 na kuanza mafunzo kwa timu zetu 2 za Taifa (wanawake na wanaume) tarehe 22/09/2012.
Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu ujio huo umesogezwa mbele, tarehe mpya ya kuwasili itatangazwa baadae mara baada ya kukamilisha taratibu husika.
Kambi ya timu ya Taifa iliyokuwa ianze tarehe 22/09/2012 kujiandaa na michuano ya kanda ya tano kwa timu za Taifa nayo imeahirishwa kwa muda hadi itakapo tangazwa tena baadae.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wote unaotokana na kusogezwa mbele kwa ujio huu wa makocha wa kigeni.
Tunachukua nafasi kuwashukuru watu wa Marekani kupitia ubalozi wao wa Tanzania ambao ndio wamekuwa wa kwanza kuutikia wito wa kusaidia maandalizi ya timu zetu za Taifa kwa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Jakaya Kikwete katika kusaidia maendeleo ya michezo hususani mpira wa kikapu.
Tunaomba wadau wengine, taasisi za umma na binafsi na wapenzi wote wa michezo na wazalendo wote mjitokeze kusaidia kwa hali na mali ili tuweze kufanikisha mipango yetu kwa faida ya vijana wetu na Taifa letu.
No comments:
Post a Comment