Rais mstaafu, Benjamin Mkapa
Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, amesema moja ya tatizo linaloifanya nchi ya Tanzania kushindwa kuwa na maendeleo inatokana na watu wengi kufanya mambo yao bila mpangilio.
Mkapa aliyasema hayo jana wakati akihutubia katika sherehe za Jubilee ya miaka 40 ya Uaskofu wa Askofu mstaafu, Mathias Isuja kwenye viwanja vya kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu mjini Dodoma.
Alisema Tanzania imekuwa ikikabiliana na matatizo mbalimbali kwa ajili ya kutafuta maendeleo licha ya watu kujifanya wajuaji wa kila kitu na kujifanya ndio wasemaji bila kufuata utaratibu.
“Siku hizi kila mtu ni mjuaji wa kila jambo na ndiyo msemaji wa kila kitu na ndiye mshauri wa kila kitu…na kufanya mambo bila ya kufuata utaratibu,” alisema Mkapa.
Aidha, alitoa wito kwa Watanzania kujifunza kutoa, kujitolea na kujituma katika kufanya kazi ili kuweza kusaidia Taifa kusonga mbele kiuchumi.
Pia, alimpongeza Askofu Isuja kwa kuweza kujitolea katika kazi zake za kiroho na kimwili kwa kusaidia waumini wake kujikwamua na hali duni walizokuwanazo kielimu, kiafya na kiuchumi.
Alimtaka askofu huyo kuendeleza yale aliyokuwa akiyafanya wakati wa watumishi wake bila kukata tamaa ili kuweza kuisaidia serikali kwa kile ambacho atakitoa katika jamii.
“Kustaafu siyo kuchoka na siyo mwisho wa uwezo wako wa kufanya kazi kila kitu kinawezakana…timiza wajibu wako,” alisema.
Kwa upande wake, askofu Isuja alitoa pongezi kwa serikali kwa kuendeleza ushirikiano na taasisi za kidini nchini.

CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Huyu mzee vipi? Na kule Kiwira kwenye mgodi wa makaa ya mawe nako alifuata utaratibu upi??
Post a Comment